Nyumbani » 09/04/2014 Entries posted on “Aprili 9th, 2014”

Tutahakikisha amani Guinea Bissau: UM

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea Bissau UNIOGBS,José Manuel Ramos-Horta

Wakati taifa la Guinea Bissau likielekea katika uchaguzi mkuu April 13 mwaka huu, Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia katika kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kabla, wakat i na baada ya uchaguzi. Katika mahojiano maalum na Monica Grayley wa idhaa ya kirusi ya Umoja wa Mataifa, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa [...]

09/04/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tutawafichua na kuwaumbua wanaofanya ukatili wa kingono: Bangura

Kusikiliza / Bi. Zainab Hawa Bangura Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili wa kingono

Mwakilishi maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili wa kingono Hawa Zainab Bangura amesema wanayopitia wanawake na watoto wanaokumbwa na ukatili wa kingono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni machungu makubwa na kazi iliyobakia sasa ni kupeperesha bendera ya kuwatetea ili kuwafuta machozi yao. Bi. Bangura amesema hayo katika mahojiano maalum [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono DRC, serikali ichukue hatua: Pillay asema!

Kusikiliza / woman DRC

Ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa pamoja na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuweka utulivu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO, zimezindua ripoti kuhusu mafanikio na changamoto katika kutokomeza ukwepaji wa sheria wa ukatili wa kingono nchini humo, ripoti hii ikitoa mapendekezo kwa wadau wote, hasa serikali ya DRC. Akizungumza [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaokoa 13 waliokuwa warejeshwe Somalia

Kusikiliza / UNHCR-logo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Kenya limesema limeweza kuwaokoa raia 13 wa Somalia waliokuwa warejeshwe makwao leo asubuhi. Naibu Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo Abel Mbilinyi ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa watu hao walikuwa miongoni mwa waliokamatwa mwishoni mwa wiki kutoka eneo la Eastleigh [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaonesha vivutio na mikakati ya kuboresha miji

Kusikiliza / Helena Mtutwa

Mkutano wa saba  kuhusu mipango miji ukiwa unaendela mjini Medellin nchini Colombia maonyesho ni moja ya vivutio ambapo nchi na taasisi mbalimbali zinaonyesha kazi na vivutio vinavyohusu ukuaji wa miji. Katika pitapita yake mwaikilishi wa  idhaa katika mkutano Joshua Mmali amekutana na mmoja wa wawakilishi wa Tanzania Helena Mtutwa ambaye ni msajili wa bodi ya [...]

09/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila dakika mwanamke hubakwa DRC

Kusikiliza / Wanawake DRC

  Ubakaji na ukatili wa kingono ni vitendo vya kihalifu ambavyo vinaendelea kutajwa huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC nchi ambayo imekabiliana na machafuko kwa muda mrefu. Matendo hayo ambayo ni ukiukwaji wa haki za biandamu yanaripotiwa zaidi mashariki mwa DRC  ambako jamii inaendelea kuteseka kwa vita. Ungana na Prscilla Lecomte katika makala [...]

09/04/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana hawataki msaada wanataka uwekezaji: Alhendawi

Kusikiliza / Ahmed Alhendawi, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Imeelezwa kuwa masuala ya vijana yanafanana kote duniani bila kujali mahali wanakotoka, na wanchotaka vijana sio msaada bali ni uwekezaji utakaowapatia fursa ya kujenga maisha. Hayo yamesemwa na Ahmad Alhendawi  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya vijana, wakati wa mkutano wa kamisheni ya Idadi ya watu na maendeleo unaojadili [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mary Robinson atembelea jimbo la Kivu Kusini na kuonyesha mshikamano na wananchi

Kusikiliza / Bi. Mary Robinson, akizungumza na Dokta Denis Mukwege wa hospitali ya Panzi huko Bukavu, ambayo hutibu wanawake waliokumbwa na ukatili wa kingono. (Picha-MONUSCO)

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za maziwa makuu Afrika, Mary Robinson amefanya ziara yake ya kwanza kabisa kwenye eneo la Bukavu, lililoko jimbo la Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako amekuwa na mazungumzo na mamlaka husika na makundi mbali mbali. Ziara hiyo ni sehemu [...]

09/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaeleza mkakati wake wa kuboresha miji

Kusikiliza / Mtaa wa mabanda, Kibera, mjini Nairobi

Mkutano wa saba  kuhusu mipango miji ukiwa unaendela mjini Medellin nchini Colombia, serikali ya Tanzania imesema inatekeleza mradi maalum wa kuboresha makazi duni ili kutimiza usawa katika makazi mijini. Mmoja wa wawakilishi wa Tanzania Hellena Mtutwa ambaye ni msajili wa bodi ya wataalamu wa mipango miji  amemweleza Joshua Mmali wa idhaa hii kuwa mpango huo [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa kina kuhusu ubia baada ya mwaka 2015 waanza UM

Kusikiliza / Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe akizungumza kwenye mkutano huo.

Hapa New York, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii wamekuwa na mjadala wa kina wa pamoja kuhusu dhima ya ubia kwenye utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015. Alice Kariuki na taarifa kamili. (Taarifa ya Alice) Maudhui ya mjadala huo ni kuangalia jinsi ubia unaweza kuongeza [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lithuania ilikiuka haki za kisiasa-UM

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Lithuania imetajwa kuvunja kwa haki za msingi za kisiasa pale ilipopitisha sheria iliyompiga marafuku kwa mtu yoyote aliyeondolewa kwenye utumishi wa umma kutowania nafasi yoyote ya uongozi, sheria ambayo ilipitishwa mara tu baada ya kuondolewa madarakani kwa nguvu kwa raia wa wakati huo Rolandas Paksas . Kulingana na kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki [...]

09/04/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasambaza misaada ya kibinadamu Syria katika hali ya tahadhari

Kusikiliza / Msaada kwa watu wa Syria

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la wakimbizi UNHRC na lile la hilali nyekundi nchiniSyriakwa mara ya kwanza limefikisha huduma za kibinadamu kwa mamia ya wakazi wa Boustan al Qaser mashariki mwa mji wa Aleppo.George Njogopa na taarifa kamili. (Taarifa ya George) Magari mawili yakiwa yamebeba vifaa mbalimbali ikiwemo mablanketi, vyakula na mahiyaji mengine yaliwasili [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tupanue mawazo ya kuendeleza nchi zetu ili yahusu miji: Prof. Stiglitz

Kusikiliza / Profesa Joseph Stiglitz

Mshindi wa tuzo ya Nobel kuhusu uchumi, Profesa Joseph Stiglitz, amesema kuwa wakati watunga sera wanapofikiria jinsi ya kuendeleza nchi zao, ni vyema vilevile kufikiria jinsi ya kuendeleza miji. Akitoa mifano ya nchi kama Singapore, ambako makazi katika taifa zima ni mijini, Profesa Stiglitz amesema serikali zinaweza kuchangia pakubwa katika kuendeleza miji. Mshindi huyo wa [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo wa tiba dhidi ya homa ya ini, Hepatitis C

Kusikiliza / hepatitis-28-july

Kwa mara ya kwanza kabisa Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa mwongozo wa tiba dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini, Hepatitis C, ugonjwa sugu ambao husababisha vifo vya  kati ya watu Laki Tatu Na Nusu  hadi Nusu milioni Kila mwaka. WHO inasema mwongozo huo umezingatia tathmini ya kina na ushahidi wa kisayansi kwa hiyo [...]

09/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031