Nyumbani » 08/04/2014 Entries posted on “Aprili 8th, 2014”

WHO : mlipuko wa Ebola ni changamoto kubwa

Kusikiliza / Idara ya Magonjwa ya Kuambukiwa - Guinea Conakry - 
@WHO - T. Jasarevic

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema leo kwamba mlipuko wa Ebola unaendelea nchini Guinea na Liberia ambapo hadi idadi ya vifo vilivyothibitishwa kutokana na ugonjwa huo ni 72 kati ya watu 108 waliofariki dunia. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mjini Geneva, Daktari Keiji Fukuda, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa afya, WHO, [...]

08/04/2014 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashuhuda waeleza madhila na kinga ya malaria Tanzania

mtoto ndani ya chandarua

Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya afya April saba, huku dhimia ikiwa kutokomeza magonjwa yanayoambukizwa kwa wadudu kama vile malaria, nchini Tanzania ugonjwa huo unatajwa kupungua kwa asilimia nane. Penina Kajura wa radio washirika Afya Fm ya Mwanza amezungumza na baadhi ya mashuhuda wa ugonjwa huo wanaoeleza madhila yake na namana ya kujikinga . Ungana naye.

08/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa na uzalishaji wahitajika katika maendeleo ya miji: Ban

Kusikiliza / miji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito hatua zichukuliwe ili kuweka mfumo mpya wa ukuaji wa miji wa karne ya 21. Katika ujumbe wake wa video kwa washiriki kwenye kongamano la 7 la kimataifa kuhusu makazi ya miji, Ban amesema mfumo huo mpya utawezesha kufikia miji endelelevu zaidi, iliyo jumuishi, yenye uzalishaji [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Muarobaini wa upangaji miji ni mfumo shirikishi : Mshiriki mkutano wa makazi ya miji Colombia

Kenya urban minister sumba

Kongamano la Saba kuhusu makazi ya miji linaendelea mjini Medellin, Colombia, likiwa limeng’oa nanga . Maelfu ya watu wanashiriki kongamano hilo, kwenye mji ambao umeshuhudia mabadiliko makubwa katika kipindi cha takriban miaka 20, na kujikwamua kutoka katika umaskini, miundo mbinu duni, uhalifu na machafuko na kuwa mji wa kisasa. Miongoni mwa watu wanaoshiriki kongamano hilo [...]

08/04/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuna hofu na kinachoendelea Burundi: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Balozi Joy Ogwu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake na kile kinachoendelea Burundi wakati huu ambapo nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwakani. Hiyo ni kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Balozi Balozi Joy Ogwu, alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mashauriano ya faragha ya wajumbe, ambapo [...]

08/04/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pillay arejelea wito wake kwa suala la Syria kuwasilishwa ICC

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Bi. Navi Pillay

Nimerejelea wito wangu kwa Baraza la Usalama kuwasilisha suala la Syria kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay akirejelea wito wake wa kwanza wa aina hiyo mwezi Agosti mwaka 2011. Pillay amesema hayo kwa waandishi wa habari baada ya kuhutubia baraza la usalama kwenye kikao cha [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ni lazima kuwashirikisha wananchi katika mipango miji: Mshiriki mkutano wa makazi ya miji Colombia

Kusikiliza / WUF7

Kongamano la Saba kuhusu makazi ya miji linaendelea mjini Medellin, Colombia, likiwa limeng’oa nanga hapo jana. Maelfu ya watu wanashiriki kongamanohilo, kwenye mji ambao umeshuhudia mabadiliko makubwa katika kipindi cha takriban miaka 20, na kujikwamua kutoka katika umaskini, miundo mbinu duni, uhalifu na machafuko na kuwa mji wa kisasa. Miongoni mwa watu wanaoshiriki kongamano hilo ni [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaeleza wasiwasi wa usalama wa chakula Syria

Kusikiliza / Syria njaa WFP

Nchini Syria kuna uwezekano mkubwa wa kutokezea hali mbaya ya ukame nchini Syria, limeonya Shirika la Chakula Duniani, WFP, katika ripoti iliyoandaliwa na wataalam wa usalama wa chakula. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte Ripoti iliyotolewa leo mjini Geneva inasema wakati msimu wa mvua unakaribia kuisha, mvua zilizonyesha hazikutosha kuhakikisha ustawi wa mazao, hasa katika mikoa [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani mauaji ya raia Kandahar

Kusikiliza / kubis

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umelaani mashambulio ya raia katika jimbo la Kandahar ambako watu 15 waliuawa na wengine watano kujeruhiwa kutokana na vilipuzi. Katika taarifa yake UNAMA inasema mnamo Aprili 7 katika kijiji cha Gilankicha katika wilaya ya Maywand ilioko Kandahr bomu ilitegwa kwenye gari ambalo lilikuwa limebeba raia ishirini, ambapo [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yasema uchumi wa CAR sasa mashakani

Kusikiliza / Hali ya uchumi ni mbaya CAR: WFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mashauriano ya faragha kuhusu hali ya usalama na haki za binadamu kwenye nchi kadhaa za Afrika na huko Mashariki ya Kati. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. Miongoni mwa nchi ambazo Baraza linajikita kuangazia ni Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo machungu kwa wananchi yanaendelea kila [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mgao wa chakula kwa wakimbizi Uganda sasa ni asilimia 100: WFP

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC walioko nchini Uganda wakipokea msaada(Picha ya maktaba)

Wakimbizi wote nchini Uganda wameanza kupokea msaada wa chakula wa asilimia mia moja kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), baada ya msaada huo kukatwa mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha. John Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchini Uganda na melezo kamili (TARIFA YA JOHN KIBEGO) Shirika la WFP [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana lazima wapewe kipaumbele ili kuondoa umaskini: Chissano

Kusikiliza / Kijana kazini

  Changamoto ya ajira kwa vijana lazima ishughulikiwe kwa kasi katika kusongesha juhudi za kupambana na umaskini hususani barani Afrika amesema rais msataafu wa Msumbiji Joaqium Chissano ambaye ni miongoni mwa wenyeviti wa mkutano wa kamisheni ya watu na maendeleo unaojadili utekelezaji wa makubaliano ya Cairo miaka 20 iliyopita. Katika mahojano maalum na idhaa hii [...]

08/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031