Nyumbani » 07/04/2014 Entries posted on “Aprili 7th, 2014”

Ban alaani mauaji ya wafanyakazi wawili wa UM

Kusikiliza / KM Ban

Katibu Mkuu a Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wawili wa ofisi ya Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC katika uwanja wa ndege wa Galkayo Puntiland Somalia. Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu mjini New York , Bwana Ban ametuma salamu za [...]

07/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tumepambana na malaria, kidinga popo kipo na juhudi zinaendelea: Tanzania

who health day

Leo dunia imeadhimisha siku ya afya, siku ambayo maudhui yake ni kutokomeza magonjwa yanayoambukizwa na wadudu mathalani malaria na homa ya denge yaani kidinga popo. Shirika la afya duniani WHO limetaka kutokomezwa kwa magonjwa hayo ambayo huathiri watu bilioni moja kote duniani na kuuwa milioni moja. Nchini Tanzania taifa hilo linaelezwa kupiga hatua katika kupunguza [...]

07/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka kuwafikia waomba hifadhi na wakimbizi waliokamatwa Nairobi

Kusikiliza / UNHCR logo

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Kenya linasikitishwa na kukamatwa kwa watu mwishoni mwa juma mjini Nairobi kufuatia mashambulizi ya kigaidi kwenye mji huo mkuu. Shughuli hizo ziliendeshwa na polisi katika maeneo ya makazi ya Eastleigh ambako wakimbizi kutoka Somalia na waomba hifadhi wanakoishi na eneo ambako mashambulizi hayo yalifanyika. UNHCR imepokea [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwait yatoa dola milioni 100 kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Mtoto aliyekimbia maeneo ya Aleppo Syria @UNHCR / A. Harper

Serikali ya Kuwait imetangaza kuchangia dola milioni 100 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, ili kusaidia wasyria. Antonia Guterres, Mkurugenzi wa UNHCR, ameshukuru Kiongozi Mkuu wa Kuwait Sheikh Sabah Al-ahmed Al-Jaber Al-Sabah, pia serikali na wananchi wa Kuwait kwa mchango wao mkubwa. Aliongeza kwamba fedha hizo zinahitajika sana kwa kuokoa maisha [...]

07/04/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tofauti zozote zinazoanza kujitokeza zishughulikiwe kuepusha mauaji:Balozi Mulamula

Kusikiliza / Logo-ICGLR

Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, bado Umoja wa Mataifa unasema kuna viashiria penginepo vya uwezekano wa kutokea mauaji ya aina hiyo ikizingatiwa yanayoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini. Je nini nchi zinapaswa kufanya? Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mtendaji wa kwanza wa Mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, [...]

07/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Fukuto za tofauti katika jamii zishughulikiwe mapema kuepusha mauaji: Balozi Mulamula

Kusikiliza / Balozi Liberata Mulamula (picha ya maktaba/UM)

Miaka 20 tangu kufanyika kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ni vyema mataifa kuchukua hatua stahili na mapema pindi kunapoibuka fukuto za misingi mbali mbali ya tofauti katika jamii, amesema Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mtendaji wa kwanza wa Mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, ICGLR. Mulamula ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani amesema [...]

07/04/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi Maalum wa UM Somalia alaanai mauaji ya wafanyakazi wa UNODC

Kusikiliza / Nicholas Kay, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Somalia

Nicholas Kay, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, amelaani mauaji ya wafanyakazi wawili wa shirika la kudhibiti uhalifu na madawa ya kulevya UNODC. Wafanyakazi wa kimataifa hawa wawili, walipigwa risasi na watu wasiojulikana, katika uwanja wa ndege wa Galkayo, Puntland, Somalia. Nicholas Kay amesema kwamba wenzao wa Umoja wa Mataifa [...]

07/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 7 kuhusu makazi ya mijini yaanza Medellin, Colombia

Kusikiliza / habitat-7

Kikao cha saba cha kongamano la kimataifa kuhusu makazi ya mijini kimeanza leo katika mji wa Medellin (Medeyin), nchini Colombia, kikivutia takriban washiriki elfu kumi na tano kutoka kote duniani. Kutoka Medellin, Joshua Mmali anaripoti:  TAARIFA YA JOSHUA Tangu mwishoni mwa wiki, washirika kwenye kongamano hili la saba kuhusu makazi ya mijini wamekuwa wakijiandikisha hapa [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM ataka Philippines ifutiwe madeni

Kusikiliza / phil-typhoon-haiyan

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Cephas Lumina ametoa wito kwa wadai wa kimataifa kuchukua hatua ya kufuta madeni yote kwa Philippines na wakati huo huo ametaka kutolewa kwa misaada isiyoambatana na masharti kwa taifa hilo ambalo linaanza kujijenga baada ya kukumbwa na kimbunga Haiyan mwaka uliopita. Mtaalamu huyo amesema kuwa Philippnes [...]

07/04/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya afya duniani, homa ya kidinga popo yaripotiwa Tanzania.

Kusikiliza / Siku ya afya duniani

Leo ni siku ya afya duniani ujumbe ukilekezwa katika kutokomeza magonjwa yanaoyo ambukizwa na wadudu kamavile malaria na kidinga popo au homa ya denge, shirika la afya duniani WHO limetaka watu kujikinga dhidi ya magonjwa hayo ambayo huathiri zadi ya watu bilioni moja na kuuwa milioni moja duniani. Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa ugonjwa wa [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi za UM chukueni hatua haraka mnapoona viashiria vya mauaji: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Tungaliweza kuchukua hatua zaidi kuepusha mauaji ya kimbari Rwanda! Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika hotuba yake kwenye kumbukizi ya miaka 20 ya mauaji hayo mjini Kigali hii leo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (Taarifa ya Alice) Hotuba ya Bwana Ban ilikuwa na kauli za kudhihirisha vile jamii ya kimataifa ilivyochelea [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Cambodia yatakiwa kuheshimu haki za binadamu

Kusikiliza / Surya Subedi

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia Surya Subedi amelaani hatua ya hivi karibuni ya bunge la taifa hilo kukutana huku wabunge wa upinzani wakikosa fursa ya kushiriki. Mjumbe huyo amesema kuwa kitendo cha bunge hilo kukutana kwa mara ya kwanza wiki iliyopita bila kuwepo kwa wabunge wa [...]

07/04/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali ya wanachi CAR inazidi kuwa mbaya-UM

Kusikiliza / car3-300x257

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu kujitokeza kwa hali mbaya zaidi ikiwemo kuporomoka kwa hali ya uchumi kutokana na machafuko yanayoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na linalohusika na mpango wa chakula duniani WFP yamesema kuwa mkwamo unaoendelea kujitokeza nchi humo kumefanya mamia ya watu [...]

07/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rwanda imepiga hatua, sasa iimarishe mahusiano mema na jirani zake:Chissano

Kusikiliza / Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chisano na Joseph Msami wa Idhaa hii

Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chisano amesema nchi hiyo imepiga hatua katika maridhiano na utengemano huku akitoa angalizo la kuimarisha amani ndani ya nchi na amani na nchi jirani. Akizungumza mjini New York, Marekani katika mahojiano maalum na Idhaa hii kuhusu kumbukizi ya miaka ishirini ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda Rais mstaafu Chissano ambaye alishiriki [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari, Rwanda yazidi kuimarika: Balozi Nduhungihere

Kusikiliza / vijana wakishikilia mwenge wa kumbukumbu, huko makao makuu ya umoja wa mataifa, New York, siku ya uzunduzi wa Kwibuka20

Leo tarehe 7, Aprili ni siku ya kumbukizi ya miaka 20 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon yupo mjini Kigali kushirikii kumbukizi hiyo. Katika salamu zake Ban amesema dunia itakumbuka daima mauaji hayo, ambapo watu 800,000 walifariki dunia. Hata hivyo amewapongeza wanyarwanda kwa kuonyesha mfano [...]

07/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031