Nyumbani » 04/04/2014 Entries posted on “Aprili 4th, 2014”

UNAMA yalaani mauaji ya waandishi wa habari Afghanistan

Kusikiliza / kubis

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afganstan UNAMA unalaani vikali shambulio la kuchukiza dhidi ya waandishi wawili wa habari wa kimataifa lililosabaabisha kifo cha mmojawao huku mwingine akijeruhiwa. Waandishi hao wawili kutoka shirika la habari la Associated Press ni ripota Kathy Gannon na mpiga picha Anja Niedringhaus na walipigwa risasi jimboni Khost mashariki mwa Afghanistan [...]

04/04/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Siku ya kujenga hamasa kusaidia watu wenye ulemavu wa akili

autism day

04/04/2014 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mgawo wa vyakula toka angani waokoa maisha ya wananchi Sudani Kusini

Kusikiliza / sudan food aid

Huku mgogoro huko Sudani Kusini ukizidi kushika kasi, Umoja wa Mataifa nao unahaha kutoa usaidizi kwa wananchi ambao wanaathiriwa na machafuko hayo na sasa wanagawa msaada kwa njia ya anga. Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte katika makala ifuatayo.

04/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto mmoja kati ya watoto 160 anakabiliwa na usonji: WHO

Kusikiliza / Nembo

Usonji! Ni tatizo la kiafya ambalo linaelezwa kusumbua watoto duniani lakini mara nyingi ni vigumu wazazi au jamii kutambua. Watoto hutelekezwa kwa kuonekana pengine ni vichaa na kubandikwa majina ya kukatisha tamaakamavile laana! Aghalabu watoto hawa kufurahia maisha kwani jamii huwatenga na shuleni nako hukataliwa. Wazazi hukumbwa na mkwamo. Takwimu za shirika la afya duniani, [...]

04/04/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wadudu waenezao magonjwa bado ni tishio: Utashi wa kisiasa wahitajika: Ban

Kusikiliza / WHO inasema mng'ato wa mbu ni mdogo lakini madhara yake ni makubwa. (Picha-WHO)

Wakati dunia inaelekea kwenye maadhimisho ya siku ya afya duniani tarehe Saba mwezi Aprili, Umoja wa Mataifa umesema magonjwa yanayoenezwa na wadudu kama vile mbu, kupe, konokono na inzi bado yameendelea kuwa tishio kwa binadamu. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa siku hiyo amesema tishio la magonjwa hayo kwa [...]

04/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM ametolea wito mamlaka za Kazakhstan kusitisha usajili wa jamii za kidini

Kusikiliza / Ramana ya Kazakhstan

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa Heiner Bielefeldt ametolea wito serikali ya Kazakhstan kusitisha  usajili wa lazima wa jumuiya za kidini kwani hali hiyo imezua hofu ya ukosefu wa usalama wa kisheria na kuathiri makundi madogo ya watu.   Amesema kwamba uwepo wa madhehebu mbali mbali ya kidini ni wa siku nyingi katika  historia ya [...]

04/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jamii zinazohifadhi wakimbizi wa Syria huko Lebanon zimezidiwa uwezo: OCHA

Kusikiliza / Bi. Valerie Amos, Mkuu wa OCHA akizungumza na watoto wakimbizi wa Syria kwenye eneo alilotembelea huko Kaskazini mwa Lebanon. (Picha: OCHA)

Mkuu wa Ofisi inayoratibu usaidizi wa kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos amehitimisha ziara yake huko Lebanon na kutaka jamii ya kimataifa kusaidia wananchi wa Lebanon wanaokumbana na changamoto kila uchao wanapohaha kukirimu wakimbizi kutoka Syria. Amesema usaidizi huo uende sanjari na usaidizi kwa wakimbizi wa Syria kwani miaka mitatu tangu kuanza kwa [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO,WFP ,IFAD wazindua mkakati wa kilimo na chakula endelevu

Kusikiliza / Vyakula tofauti sokoni

Mashirika ya chakula na kilimo lile la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na mpango wa chakula duniani WFP, leo yamezindua matokeo ya ushirikiano wa mashirika hayo katika kuendeleza malengo na viashiria kwa ajili ya kielelezo cha maendeleo endelevu kimataifa katika kilimo, usalama wa chakula [...]

04/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tunaposhughulikia majanga tusisahau ajenda muhimu za dunia: Ban

Kusikiliza / Katibu mkuu Ban Ki-Moon akitoa mhadhara kwenye Chuo Kikuu cha Charles mjini Prague, Jamhuri ya Czech.

Kadri tunavyokabiliana na majanga ya Ukraine, Syria, Sudan Kusini na ukatili huko Jamhuri ya Afrika ya Kati hatupaswi kusahau mambo muhimu ambayo yanaweza kuonekana hayana uharaka lakini ni vitisho vya muda mrefu iwapo yatapuuzwa. Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika mhadhara aliotoa leo kwenye Chuo Kikuu cha Charles huko Prague, Jamhuri [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wananchi wamechoka na vita, wanatoa taarifa za uhalifu CAR: UM

Kusikiliza / CAR watu wamechoka

Wakati ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetembelea manusura wa tukio la mashambulizi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambapo kundi la Anti Balaka liliwashambulia askari walinda amani kutoka Chad, mwenyekiti wa tume ya kimataifa ya uchunguzi Benard Muna amesema watu wa CAR wamechoka na machafuko nchini humo. Taarifa zadi na [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

James Bond aungana na UNMAS kuhamasisha kuhusu madhara ya mabomu ya kutegwa ardhini

Kusikiliza / mine

Leo ni siku ya kimataifa ya uhamasishaji na kutoa msaada wa kutokomeza matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini ambapo maudhui yake yanaangazia umuhimu wa wanawake katika shughuli hizo. Grace Kaneiya na Taarifa kamili. Katika ujumbe wake wa siku hii, Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema ni muhimu wanawake washirikishwe zaidi katika [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afghanistan sasa inaandika historia: UNAMA

Kusikiliza / Afghanistan elections

Wakati wananchi wa Afghanistan kesho wanapiga kura katika uchaguzi wa Rais na viongozi wa majimbo, mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubis amesema historia imeanza kuandikwa. Amesema historia inaandikwa kwani kwa mara ya kwanza mamlaka za uchaguzi nchini humo zikiwemo zile za serikali kuu na majimbo zinawajibika kwa asilimia mia [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hukumu ya kifo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, Somalia:OHCHR

Kusikiliza / Rupert Colville OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa, OHCHR imepokea taarifa za kuuawa kwa mwanamume mmoja Aprili 3 mjini Kismayo , Somalia baada ya kutuhumiwa kumuua mzee mmoja mwezi uliopita. Mtuhumiwa alipatwa na hatia wiki iliyopita lakini haijulikani hukumu hiyo ilitolewa na nani na kuna uwezekano haikutolewa na mahakama. Kulingana na taarifa ilizopokea ofisi [...]

04/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930