Nyumbani » 02/04/2014 Entries posted on “Aprili 2nd, 2014”

CAR, UNAMID miongoni mwa masuala ya kuangaziwa na Baraza la Usalama Aprili

Kusikiliza / Joy Ogwu, Mwakilishi wa Kudumu wa Nigeria kwenye Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa ratiba yake ya masuala muhimu yatayoangaziwa katika vikao vyake mwezi huu wa Aprili. Nigeria ndiyo inayoshikilia kiti cha urais wa Baraza hilo mwezi huu wa Aprili. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York baada ya kikao chake leo, Mwakilishi wa Kudumu wa Nigeria kwenye Umoja wa [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unywaji pombe wahatarisha afya ya wajawazito na watoto

Kusikiliza / wanawake wajawazito

Malengo ya maendeleo ya milenia yanafikia ukomo mwakani. Miongoni mwa malengo hayo ni lile nambari Tano linalosisitizia afya ya wajawazito ili mtoto anayezaliwa awe na afya bora na hata mama mzazi. Lakini hali inaonekana kukumbwa na mkwamo kiasi kwa baadhi ya familia huko Mwanza ambako mjamzito mmoja anakunywa pombe kupita bila kujua madhara yake kama [...]

02/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za wanawake na wasichana Afghanistan ziimarishwe zaidi

Kusikiliza / Wanawake nchini Afghanistan. (Picha-UNAMA)

Ari ya wanawake wa Afghanistani ya kutaka amani na kusitishwa mapigano nchini humo ni lazime iendelezwe! Amesema Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA Ján Kubiš. katika taarifa iliyomnukuu akirejelea ombi lililotiwa saini na zaidi ya wanawake na wasichana 250,000. Kubiš amesema suala kwamba andiko hilo limeandaliwa na kukusanya kiasi hicho cha [...]

02/04/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tetemeko la ardhi Chile limejibiwa vizuri na serikali: UM

Kusikiliza / map Chile

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza athari za majanga UNISDR kwa ukanda wa Marekani Kusini na Karibia, Ricardo Mena, amesema leo kwamba serikali ya Chile imepambana vizuri na tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo jumanne usiku, tarehe 2, April. Tetemeko hilo lililotokea maeneo ya Iquique, kaskazini mwa Chile, limefikia kiwango cha 8.2 [...]

02/04/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kituo cha Gabriella na Autism Connects Tanzania waleta nuru kwa watoto wenye Usonji

Kusikiliza / Hafla ya maadhimisho ya siku ya Usonji

Aprili Pili ni siku ya kimataifa ya Usonji. Dunia imekuja pamoja kwa ajili ya kuhamasisha jamii na kuelimisha kuhusu ugonjwa huo ambao mbali na changamoto ya huduma ya afya hususan katika mataifa yenye kipato cha chini, kuna pengo uelewa juu ya ulemavu wa akili au usonji. Katika mahojiano maalum na Idhaa hii Brenda Shuma, Mkurugenzi [...]

02/04/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yamulika mabadiliko ya tabianchi, utapia mlo na kilimo cha kaya

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva, wakati akilihutubia kongamano la kikanda la Ulaya mjini Bucharest, Romania.

Athari za mabadiliko ya tabianchi katika uzalishaji wa chakula zimemulikwa katika hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva, wakati akilihutubia kongamano la kikanda la Ulaya, ambalo limehudhuriwa na nchi 46 mjini Bucharest, Romania.   Akiangazia ripoti iliyotolewa wiki hii na Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, [...]

02/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria Lebanon wanakabiliwa na mazingira magumu ya kazi: ILO

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon wanakabiliwa na mazingira ngumu ya kazi

Ripoti hiyo inasema kuwa wakimbizi wa Syria nchini Lebanon pia wanafanya kazi katika mazingira magumu na kulipwa mishahara midogo. Wakati huo huo ripoti hiyo inaonyesha kwamba wakimbizi hao wanakosa ujuzi na elimu. Wanawake hasa wanakabiliwa na ukosefu wa ajira huku zaidi ya theluthi mbili ya wanawake wanaotafua kazi wakishindwa kupata ajira. Idadi kubwa ya wakimbizi [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kati ya Afrika na Ulaya Brussels : Ban aomba mshikamano

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa Brussels

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amehudhuria mkutano wa vongozi wa Muungano wa Ulaya na Muungano wa Afrika huko Brussels, Ubelgiji na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano na upendo kati ya pande mbili hizo hususan suala la wahamiaji. Bwana Ban ametoa hotuba kwenye kikao hicho cha siku mbili kitakachomalizika kesho. (Sauti ya Ban) [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito kwa nchi wanachama wa UM kuridhia mkataba wa biashara ya silaha

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson(picha ya maktaba)

Ikiwa leo ni umetimu mwaka mmoja tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha mkataba wa kihistoria kuhusu biashara katika silaha, imefanyika hafla ya kuadhimisha kupitishwa kwa mkataba huo hapa kwenye Umoja wa Mataifa, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, akitoa wito kwa nchi wanachama kuridhia mkataba huo bila kuchelewa. Taarifa kamili [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uelewa kuhusu usonji bado mdogo, wenye usonji huitwa vichaa:

Kusikiliza / Hafla ya maadhimisho ya siku ya Usonji duniani Aprili 2

Fikra potofu na imani za kishirikina ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kukwamisha juhudi za kitabibu za kuokoa watoto wenye usonji au ulemavu wa akili nchini Tanzania. Ni kauli aliyotoa Brenda Shuma, Mkurugenzi wa Kituo cha Gabriella kilichoko mkoani Kilimanjaro alipozungumza na idhaa hii leo siku ambayo ni ya kimataifa ya kuhamasisha elimu juu ya ulemavu [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kushirikiana na Uganda na DRC kurejesha wakimbizi makwao

Kusikiliza / Waimbizi wa kutoka DRC walioko nchini Uganda waliohudhuria mkutano wa swala la urejeshaji nyumbani kwa ushirikiano wa seriklai na UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na serikali zaUgandana Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanandaa kurejesha nyumbani takribani wakimbizi Laki moja na Elfu Themanini wa DRC walioko nchiniUganda. Hatua hiyo inafuatia kifo cha wakimbizi 108 wa DRC waliozama katika Ziwa Albert wakati wajirejea nyumbani kivyao kutoka kambi moja nchiniUgandamwezi [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tupatie ubongo wetu lishe bora kama tunavyolisha miili yetu:

Kusikiliza / Autism

Wakati ulimwengu leo unaadhimisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha vitendo kuhusu ulemavu wa akili kwa kuwasha mwanga wa bluu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kadri siku zinavyosonga, watoto na watu wazima wenye ulemavu wa akili wanazidi kutengwa na jamii zao na hata katika jamii ambako wanajumuishwa bado wanakosa huduma za msingi. [...]

02/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930