Ujasiri wamwezesha Isca kujikita katika biashara iliyotawaliwa zaidi na wanaume

Kusikiliza /

Isca Kauga-Joshua

Kauli ya Umoja wa Mataifa ya kwamba usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote imethibitika kwa mtanzania Isca Kauga-Joshua aishie Marekani aliyeamua kuvunja mipaka ya biashara ya upigaji picha za mnato na video iliyotawaliwa zaidi na wanaume ambayo sasa amesema imemwezesha kuboresha maisha yake na familia yake.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mdau mshirika wa Idhaa hii Sunday Shomari, Isca amesema awali alikuwa na hofu kuacha ajira na kujiajiri lakini nia ya kuvunja mpaka huo ilimfungulia njia.

(Sauti ya Isca)

Isca amesema kwa sasa ameweza kupanua wigo wa wateja wake ndani na nje ya Marekani ambako anaishi na kutokana na uaminifu wake ameweza kukubalika na mtandao ndio umemwezesha.

(Sauti ya Isca)

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930