Ombi la misaada ya kibinadamu Syria limefadhiliwa kwa asilimia 9 tu: OCHA

Kusikiliza /

Kambi ya kuwahifadhi wakimbizi wa Syria (Picha ya UNHCR)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo linafanya mkutano wa faragha kuhusu hali nchiniSyria, wakati Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, ikisema kuwa kuna uhaba wa ufadhili kwa mashirika yote ya kibinadamu yanayohudumu nchini humo  na katika nchi jirani kuliko wakimbizi. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

Ombi lililotolewa kwa ufadhili wa huduma za kibinadamu ndani yaSyriani dola bilioni 2.2, lakini mashirika ya kutoa huduma hizo yamepokea asilimia 9 tu ya fedha hizo. Msemeji wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, Jens Laerke, amesema licha ya ahadi za ufadhili mapema mwaka huu, bado kwa ujumla ufadhili upo chini

JENS LAERKE

"Tulikuwa na kongamano la kutoa ahadi za ufadhili mnamo mwezi Januari nchini Kuwait, na ahadi zilitolewa za zaidi ya dola bilioni 2, lakini kufikia sasa ni asilimia 22 tu ya ahadi hizo zimetimizwa na kutolewa, kwa hiyo chini ya robo"

Katika nchi jirani zinazowahifadhi wakimbizi waSyria, ni asilimia 14 tu dola bilioni 4.4 ndizo zimepatikana

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031