Mahitaji ya maji yaongezeka kutokana na mahitaji ya nishati

Kusikiliza /

 

Siku ya maji duniani

Umoja wa Mataifa unaadhimisha tarehe 22 siku ya kimataifa ya maji, ikilenga jinsi maji na nishati zinaambatanishwa.

Chombo kinachoratibu masuala ya maji na usafi katika umoja wa mataifa, UN Water, kimesema kwamba maji yanahitajika katika kutengeneza aina zote za nishati. Pia nishati inahitajika kwa upatikanaji na usafishaji wa maji.

UN Water imeongeza kuwa ongezeko la mahitaji ya nishati yanasabibisha mahitaji ya maji yaongezeke pia. Awali, mabadiliko ya tabia nchi yanatokanayo mara kwa mara na matumizi mabovu ya nishati, yanaleta mvutano mkubwa zaidi wa upatikanaji wa maji.

Michel Jarraud ni Mwenyekiti wa UN Water.

"Mahitaji ya maji kwa ajili ya kutengeneza nishati yanaongezeka na yanasababisha ushindani baina sekta ya nishati na sekta nyingine zinazohitaji maji kama kilimo au viwanda.  Tukitaka kujenga maisha endelevu kwa baadaye, inabidi tuwezeshe upatikanaji wa maji kwa njia mwafaka na endelevu kwa watu zaidi ya bilioni 1.3 wanaoishi bila umeme na kwa watu zaidi ya milioni 700 ambao bado hawapati maji kwa njia bora". 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031