Ban akutana na Waziri Mkuu wa Ukraine

Kusikiliza /

Ban na Yatsenyuk

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk mjini Kyiv.

Wametathmini kuhusu hali ya sasa nchini Ukraine na ukanda mzima. Katibu Mkuu amempongeza Waziri huyo Mkuu kwa hotuba yake ya hivi karibuni ambapo alitoa wito kuwepo harakati  jumuishi za kisiasa nchini Ukraine. Bwana Ban pia amesisitiza ujumbe wake kwamba ni suluhu la kidiplomasia pekee linalotokana na misingi ya Katiba ya Umoja wa Mataifa ndilo litautatua mzozo uliopo sasa kati ya Urusi na Ukraine.

Katibu Mkuu pia amemweleza Waziri Mkuu Yatsenyuk kuhusu mkutano wake wa hivi karibuni na viongozi wa Urusi, wakiwemo Rais Putin na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergey Lavrov. Bwana Ban amesema mazungumzo ya moa kwa moja kati ya Ukraine na Urusi ni muhimu katika kupunguza utata uliopo sasa.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031