Nyumbani » 25/03/2014 Entries posted on “Machi 25th, 2014”

UNSOM yalaani mauaji ya viongozi wa kaya Somalia

Kusikiliza / UNSOM alaani mauaji ya viongozi Baidoa

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Somalia, Nicholas Kay, amelaani vikali mauaji ya viongozi wa kaya wanane pamoja na mashumbulizi kati ya vikundi tofauti vinavyodai kuwakilisha serikali, yaliyotokea jana Baidoa, kusini mwa Somalia. Ametuma rambirambi zake kwa familia na jamii za waliouawa akisisitiza umuhimu wa uchunguzi ili waliotekeleza uhalifu huo wahukumiwe ipasavyo. Kwa mujibu wa [...]

25/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pamoja na kukumbuka utumwa, tumulike utumwa wa sasa na kuutokomeza: Dtk. Ashe

Kusikiliza / Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Dkt. John william Ashe

Tukio maalum la kukumbuka wahanga wa utumwa na wa biashara ya utumwa kupitia Atlantiki limefanyika kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne siku ya kimataifa ya kukumbuka tukio hilo. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ushindi dhidi ya utumwa:Haiti na kwingineko. Rais wa Baraza Kuu Dkt. John William Ashe akizungumza kwenye tukio [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aisisitiza kumalizwa kwa mgogoro wa Ukraine kwa njia za kidiplomasia

Kusikiliza / Katibu Mkuu pamoja na Waziru Mkuu wa Uingereza

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amesisitiza kuwa mgogoro kati ya Ukraine na Urusi kuhusu jimbo la Crimea utamalizwa kwa njia za kidiplomasia pekee. Ban ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron mjini The Hague Uholanzi ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kupunguza [...]

25/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shughuli za kilimo zapigwa jeki kufuatia mafunzo kwa wakulima Somalia

Kusikiliza / Zao la mahindi

Wakulima nchini Somalia wana furaha kwani kwa mara ya kwanza wameweza kuzalisha chakula cha kiwango cha juu na kulisha jamii, hii ni habari njema ikizingatiwa kwamba nchi hii imekumbwa na mzozo kwa miongo miwili huku ikifanya ikifanya kilimo ambacho ni uti wa mgongo Afrika kusahaulika basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo.

25/03/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan na Sudan Kusini sasa zimesahaulika, watoto wahoji matunda ya uhuru: Ging

John Ging

Kadri mizozo na majanga yanavyozidi kuibuka maeneo mengine duniani, mustakhbali wa wakazi wa Darfur huko Sudan unazidi kutoweka huku nchini Sudan Kusini watoto wanahoji yalikoenda matarajio ya matunda ya uhuru wa taifa lao changa. Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyosemwa na viongozi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA walipozungumza [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za binadamu lamulika ukatili wa kingono DRC.

Kusikiliza / MATIPA

Baraza la haki za binadamu leo limepokea ripoti kuhusu ukatili wa kingono huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo limetaka hatua zichukuliwe kusaidia wahanga. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Akihutubia kikao hicho, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema ukatili wa kingono bado unafikia hatua [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na wadau waendelea na usaidizi wa kiutu kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Msafara wa malori yakiwa yamebeba misaada ya kibinadamu yakielekea Syria kutoka Uturuki (picha ya OCHA, maktaba)

Umoja wa Mataifa na wadau wake wameendelea kutoa usaidizi kwa wananchi wa Syria wanaoendelea kukumbwa na madhila kufuatia mapigano yanayoendelea nchini mwao huu ukiwa ni mwaka wa nne sasa. Umoja huo kupitia ofisi yake ya kuratibu misaada ya kiutu, OCHA leo umetangaza kuwa malori 12 hatimaye yameweza kuingia Syria kutoka Uturuki yakiwa yamesheheni vyakula na [...]

25/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kizungumkuti Sudan Kusini chazidi, dola Milioni 371 zahitajika kwa usaidizi

Kusikiliza / Mahitaji ya kibinadamu ya watu wa Sudan Kusini ni mengi, UNHCR

Wakati hali ya usalama na kibinadamu ikizidi kuzorota huko Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ya kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la mpango wa chakula WFP yametoa ombi la usaidizi wa dola Milioni 371 ili kuimarisha huduma zao kwenye eneo hilo. Ombi hilo linawakilisha pia mahitaji ya wadau wengine wanaoshirikiana na mashiriak hayo [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkurupuko wa Ebola Guinea-Conakry waua watu 59, WHO, EU yasaidia uchunguzi na tiba

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema watu 59 wamefariki dunia kutoka na ugonjwa wa Ebola huko Guinea-Conakry, huku likitanabaisha kuwa uchunguzi dhidi ya watu waliokuwa wanashukiwa kuwa na ugonjwa huo huko Canada umebaini kuwa si Ebola. Taarifa zaidi na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Sintofahamu ya kuibuka kwa ugonjwa huo imeibuka mwishoni mwa wiki ambapo [...]

25/03/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watiwa hofu na idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa Misri

Kusikiliza / UM watiwa hofu na idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa Misri

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza hofu yake juu ya idadi kubwa ya watu waliohukumiwa adhabu ya kunyogwa hadi kufa nchini Misri. Hukumu hiyo ya Jumatatu ni dhidi ya watu 528 na ilitolewa baada ya kesi yao kusikilizwa kwa siku mbili. Ofisi ya haki za binadamu inasema kesi hiyo haikukidhi viwango [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu tusisahau yaliofanyika utumwani ili yasishuhudiwe tena:Ban

Kusikiliza / Slave trade

Leo Machi 25 ni siku ya Kimataifa ya maadhimisho ya siku ya utumwa na biashara ya utumwa. Siku hii huadhimishwa kila mwaka na imetengwa kwa ajili ya kutoa fursa ya kuwaenzi na kuwakumbuka watu walioteseka na kufa mikononi mwa mfumo kandamizi wa utumwa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Ushindi dhidi ya utumwa:Haiti na kwingineko. [...]

25/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031