Nyumbani » 24/03/2014 Entries posted on “Machi 24th, 2014”

Uchafuzi wa hewa wasababisha vifo vya watu Milioni Saba duniani kote: WHO

Kusikiliza / climate change

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa makadirio mapya ya vifo vya binadamu vitokanavyo na uchafuzi wa hali ya hewa ambapo mwaka 2012 pekee watu Milioni Saba walifariki dunia. WHO inasema ripoti hiyo mpya inaweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa ni moja ya athari kubwa zaidi ya afya itokanayo na uchafuzi wa mazingira na kwamba kupunguza [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa Intaneti waweza kupunguza umaskini

Kusikiliza / africa-youth-broadband

Mtandao wa Intaneti unaotumia kuhamisha-data kasi (broadband Internet) unafaa kuangaliwa kama nyenzo ya msingi ya kuleta maendeleo, kwa mujibu wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kidigitali, iliyokutana mwishoni mwa wiki iliyopita, mjini Dublin, nchini Ireland.   Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo, Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesisitiza umuhimu wa kihamisha-data kasi kwa kuinua uchumi wa nchi zinazoendelea, [...]

24/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini ya Kisiasa Haiti, Kipindupindu kinadhibitiwa: UM

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Haiti na mkuu wa MINUSTAH, Sandra Honoré

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa kuhusu hatua muhimu zinazoendelea nchini Haiti zinazoimarisha harakati za uchaguzi baadaye mwaka huu. Wajumbe wamesikiliza ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyosomwa na mwakilishi wake maalum nchini humo Sandra Honoré ambaye amesema maridhiano ya hivi karibuni baina ya jamii tofauti yamewezesha kutiwa saini kwa [...]

24/03/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yazungumzia kuzama kwa wakimbizi wa DRC huko Uganda

Kusikiliza / Safari za boti (Picha-UNHCR)

Taarifa za kuzama kwa boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliokuwepo kwenye kambi ya Kyangwali nchini Uganda imeibua simanzi huku Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, ukieleza kuhuzunika na kushtushwa na taarifa hizo. Boti hiyo ikiwa na mamia ya wakimbizi hao wakiwemo watoto ilizama Jumamosi kwenye [...]

24/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la FAO Tunis laangazia uboreshaji wa kilimo

Kusikiliza / Mama mkulima nchini Mozambique

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO, limewaomba viongozi wa Afrika wahamasishe uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuondoa njaa barani humo.Ombi hilo limetolewa katika Mkutano wa 28 wa  ukanda wa Afrika, mjini Tunis, Tunisia ambao umeanza Jumatatu. Afrika ndilo bara ambalo bado linatatizika katika kukabiliana na njaa, ukosefu wa chakula na vipato vidogo vijijini, [...]

24/03/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WaSyria waliokimbilia Lebanon wanaishi maisha ya sintofahamu

Kusikiliza / Mama na mwanawe, wakimbizi wa Syria waliokimbilia nchini Lebanon

Huku mzozo wa Syria ukiwa umeingia mwaka wa nne Machi 15, mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yamefika eneo la Bekaa mashariki mwa Lebanon ili kukutana na familia za waSyria  ambako zaidi ya wakimbizi elfu moja wametafuta hifahi. Basi ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo

24/03/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Teknolojia mpya yasaidia kuharakisha uchunguzi dhidi ya TB:WHO

Kusikiliza / World TB Day

Leo ni siku ya Kifua Kikuu duniani ambapo Shirika la Afya ulimwenguni, WHO linasema ujumbe mkuu ni kufikia watu Milioni Tatu walio kwenye mazingira magumu ya kuchunguza vyema afya zao kama njia muhimu ya kudhibiti ugonjwa huo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Idadi hiyo kwa mujibu wa WHO ni theluthi Moja ya [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takriban wakimbizi 200 wa DRCwaangamia kwenye ajali ya boti Uganda

Kusikiliza / boat uganda

Takribani wakimbizi mia mbili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamefariki dunia baada ya ajali ya mashua magharibi mwa nchi jirani ya Uganda. Wakimbizi hao walikuwa wakitoka kambi ya Kyangwali kurejea makwao bila ridhaa ya UNHCR na serikali ya Uganda siku ya Juma mosi. Kwa sasa UNHCR na serikali ya Uganda wanajikita kuodoa maiti [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wakutana The Hague kujadili hatua za kuzuia ugaidi wa nyuklia

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Viongozi wa kimataifa wanakutana mjini The Hague, Uholanzi, kujadili hatua zilizopigwa katika kuzuia ugaidi wa kutumia miyale ya nyuklia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban- Ki-Moon anatarajiwa kuhutubia kikao cha ufunguzi kwenye mkutano huo wa siku mbili unaowaleta pamoja zaidi ya viongozi 50 wa kimataifa. Mkutano huo unalenga kuhakikisha ushirikiano mahsusi wa kimataifa ili [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yapatia hifadhi maelfu ya raia waliokimbia mashambulizi Darfur

Kusikiliza / Mama na mwanae katika moja ya makazi ya muda baada ya makazi yao kuteketezwa na mali zao kuporwa. (Picha-UNAMID)

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa unaolinda amani huko Darfur, Sudan, UNAMID, umewapatia hifadhi takribani wakimbizi wa ndani 2,000 waliokimbia makazi yao ya muda kutokana na mapigano ya hivi karibuni zaidi. Raia hao wanahifadhiwa kwenye vituo vya kikoshi hicho huko Korma na Khor Abeche. Inaelezwa kuwa siku ya Jumamosi watu [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WMO yatoa ripoti kuelezea mabadiliko ya tabia nchi

Kusikiliza / Nasa

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la hali ya hewa duniani imeutaja mwaka uliopita wa 2013 kuwa ni wa majanga mazito kwa dunia ukishuhudia matukio kama ukame, mabadiliko ya hali ya hewa na kujitokeza kwa vimbunga vilivyosababisha uharibifu mkubwa wa mali. Ripoti hiyo pia matukio yaliyojitokeza mwaka huo uliopita yanafanana kabisa na matukio mengine yaliyojitokeza mwaka [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya sheria ya kunyonga inategemea maoni ya wananchi: Tanzania

Kusikiliza / Sheria ya kunyonga inategemea maoni ya wananchi wa Tanzania

Wakati mkutano wa baraza la haki la Umoja wa mataifa ukiendelea mjini GenevaUswisi, Tanzaniaimesema ufutwaji wa hukumu ya kunyonga nchini humo kunategemea maoni ya wananchi na kwamba mchakato huo unaendelea licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa. Akizungumzia ripoti ya hali ya haki za binadamu iliyowasilishwa katika mkutano huo, mwakilishi wa kudumu waTanzaniakatika ofisi za [...]

24/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Teknolojia mpya yasaidia kuharakisha uchunguzi dhidi ya TB:WHO

Kusikiliza / Tiba dhidi ya Kifua Kikuu huhusisha matumizi ya mchanganyiko wa dawa.

Leo ni siku ya Kifua Kikuu duniani ambapo Shirika la Afya ulimwenguni, WHO linasema ujumbe mkuu ni kufikia watu Milioni Tatu walio kwenye mazingira magumu ya kuchunguza vyema afya zao kama njia muhimu ya kudhibiti ugonjwa huo. Idadi hiyo kwa mujibu wa WHO ni theluthi Moja ya watu wote wanaoambukizwa Kifua Kikuu duniani kila mwaka. [...]

24/03/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031