Nyumbani » 19/03/2014 Entries posted on “Machi 19th, 2014”

Mzozo wa Ukraine-Urusi unabadilika kutoka kisiasa kuwa wa kijeshi: Eliasson

Kusikiliza / Naibu KM Jan Eliasson

Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akielekea Urusi na Ukraine kwa ajili ya kusaka suluhu la kidiplomasia kwenye mzozo wa pande mbili hizo juu ya Crimea, baraza la usalama limeelezwa kuwa mambo yanayojitokeza kila uchwao kwenye eneo hilo yanaweza kuzorotesha amani zaidi huku hali ya haki za binadamu Ukraine na Crimea ikielezwa [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake lazima washiriki uchaguzi Afghanistan : UM

Kusikiliza / Wanawake nchini Afghanistan

    Lazima wanawake washirikishwe katika Uchaguzi wa rais na wa halmashauri za kata Afghanistan ili kuhakikisha uchaguzi huo ni wazi na huru, amesema Nicholas Haysom, akiwa ni Naibu Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na Makamu wa Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa UNAMA.    Bwana Hayson amesema amefurahi [...]

19/03/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makabila asilia yapaza sauti New York

Kusikiliza / Baadhi-ya-Wamasai-wakicheza-ngoma-zao

Mkutano wa hali ya wanawake CSW ukiendelea mjini New York makabila asilia yanazidi kupaza sauti zao kuhusu haki zao za kimsingi matahalani elimu, na huduma nyingine za kijamii. Akiwa mitaani mjini humo Joseoph Msami wa idhaa hii amekutana na miongoni mmoja wa wamasai kutoka nchiniTanzania, ungana naye  

19/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na wadau warejesha nuru ya maisha kwa Arafa Halfani Mwamba:

Kusikiliza / Arafa Halfani Mwamba akifunga paneli ya umeme nishati ya jua kwenye moja ya paa la nyumba huko Mtwara. (Picha-UN-Women)

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la masuala ya wanawake, UN-Women na shirika la kujitolea la Uingereza VSO limerejesha nuru ya maisha kwa mkazi wa Mtwara nchini Tanzania, Arafa Halfani Mwamba ambaye akiwa na umri wa miaka 40 maisha yake yalitwama kutokana na ndoa iliyogeuka machungu. Kilimo cha familia hakikuwa na maslahi kwake hadi Umoja [...]

19/03/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Unesco yalaani mauaji ya wanahabari wawili Syria

Kusikiliza / stop killing journalists

Mkurugenzi mkuu wa shirika la  Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova amelaani mauaji ya waandishi wawili nchini Syria Abdul Quader na Ali Mostafa na kurejelea umuhimu wa watu kupata taarifa kama sehemu ya kutatua mgogoro. Bi Bokova ametaka pande zote nchiniSyriakusaidia waandishi wa habari katika kutimiza majukumuyaokuripoti katika mazingira [...]

19/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dokta Kelemu miongoni mwa washindi wa tuzo ya UNESCO na L'Oreal

Kusikiliza / Dkt. Segenet Kelemu

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na taasisi ya L'Oreal leo wanaendelea na utaratibu wao wa kila mwaka wa kuwapatia tuzo wanawake watano wanasayansi kila mwaka kutokana na mchango wao utafiti kwenye jamii zao. Wanawake hao, mmoja kutoka kila bara wanawakilisha mwelekeo wa kipekee wa kitaalamu ndani ya [...]

19/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ujenzi wa amani baada ya migogoro waangaziwa katika Baraza la Usalama

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Milipuko ya machafuko ya hivi karibuni katika Sudan Kusini na Jamhuri ya afrika ya Kati ni ishara dhahiri ya mazingira yasotabirika katika ujenzi wa amani, na hatari zinazohusika na harakati hizo. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama, ambalo limekutana kujadili suala la [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima wanawake Afrika bado hawajasaidiwa-Ripoti

Kusikiliza / Mwanamke mkulima

Ripoti mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema bara la Afrika liweke usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo iwapo ina nia ya dhati ya kuondokana na umaskini.  Ripoti hiyo inatokana na utafiti katika nchi za Afrika zikiwemo Ethiopia, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzaniana Uganda ambapo uliangalia tofauti ya uzalishaji baina ya wakulima wanawake na wanaume [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takriban 200,000 wajawazito Syria wahitaji huduma za dharura: UNFPA

Kusikiliza / Pregnant women Syria

Wakati mzozo wa Syria unapoingia mwaka wa nne Shirika la Idadi ya Watu katika Umoja wa Mataifa limetoa wito wa msaada wa dharura ili kuokoa maisha ya akina mama wapatao 200,000 wajawazito nchini humo, wakiwemo 1,480 ambao hujifungua kila siku katika mazingira hatarishi. Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wanawake kutokana na mgogoro wa Syria na [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo Ukraine-Crimea, Katibu mkuu Ban aelekea Urusi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anaondoka mchana huu kuelekea Urusi na baadaye Ukraine ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za diplomasia za kuhimiza pande kwenye mzozo unaoendelea kupatia suluhu kwa njia ya amani. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (Taarifa ya Alice) Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa ziara yake [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makundi madogo katika jamii bado yapuuzwa: Mtaalamu wa UN

Kusikiliza / Rita Izsák

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za makundi madogo kwenye jamii, ametaka kuchukuliwa kwa hatua zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazokabili makundi hayo ambayo amesema yako hatarini kukumbana na vitendo kama vile vya ubaguzi, kukosa fursa za kiuchumi na kukabiliwa na umaskini. George Njogopa na ripoti kamili. (Taarifa ya George) Mtaalamu huyo Rita [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wananchi Sudan wanataka maisha yenye utu: Ging

Kusikiliza / Wakimbizi wapya wa ndani huko jimbo la Darfur Kusini wakiwa wamekimbia mapigano kwenye maeneo yao.

Jopo la wakurugenzi kutoka chombo cha ubia katika masuala ya dharura baina ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia limehitimisha ziara yake ya siku tano huko Sudan kwa kutaka pande zote husika katika mapigano yanayoendelea kwenye baadhi ya majimbo nchini humo kusitisha mapigano na kuingia katika mchakato wa siasa. Jopo hilo likiongozwa na John [...]

19/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031