Nyumbani » 17/03/2014 Entries posted on “Machi 17th, 2014”

Hakujashuhudiwa mlipuko wowote kuhusu ndege ya Malaysia: CTBTO

Kusikiliza / Stephane Dujarric

Shirika la Kupinga majaribio ya Nyuklia, CTBTO, ambalo linaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, limethibitisha kuwa halijashuhudia dalili zozote za kulipuka au kishindo chochote ambacho kinaweza kuhusiswa na kutoweka kwa ndege ya Malaysia. Ndege hiyo namba MH 370 ilitoweka yapata zaidi ya wiki moja ilopita, ikiwa imewabeba watu 239 kwenye safari ya kutoka Kuala Lumpur [...]

17/03/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Iran yaombwa iongeze umri wa kuwawajibisha watoto kisheria kwa uhalifu

Kusikiliza / Nembo ya UNICEF

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limetiomba serikali ya Iran ipandishe umri wa kuwawajibisha watoto kwa makosa yanayohesabiwa kuwa ya uhalifu. Kwa sasa, watoto wa kike wenye umri wa miaka 9 na wavulana wa umri wa miaka 15 wanaweza kuwajibishwa kisheria kwa makosa ya uhalifu. Iran imefanyia marekebisho kanuni zake za Kiislamu [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bila kuwashirikisha wasichana hakuna maendeleo:Washiriki CSW

Kusikiliza / Bi Mary Makungwa

Mkutano maalum kuhusu sauti ya wanawake na wasichana kutoka Afrika umefanyika leo mjiji New York ambapo wawakilishi kutoka bara hilo na kwingineko wamesema bila kuwawezesha watoto wa kike haiwezekani kutimiza lengo namba tatu la kuwezesha wanawake na usawa wa kijinsia. Katika mahojiano maalum na idhaa hii miongoni mwa waliowasilisha mada waziri wa jinsia kutoka Malawi [...]

17/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usafi wa sikio waangaziwa

Kusikiliza / Usafi wa sikio

Usafi na utunzaji wa sikio ni suala muhimu sana katika afya ya binadamu kwani kwa mara nyingi watu hawana habari sahihi kuhusu namna ya kutunza au kusafisha sikio. basi ungana na John Kibego wa Radio washirika spice Fm nchini Uganda katika ripoti ifuatayo.  

17/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa daftari la takwimu kuhusu ardhi duniani

Kusikiliza / Ardhi

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO limetoa takwimu kuhusu hali jumla ya ardhi na matumizi yake kupitia daftari la takwimu kuhusu matumizi ya ardhi, SHARE inayotoa maelezo kuhusu ni kiasi gani cha ardhi kinatumika kwa mfano kwa mimea, miti au ardhi ambayo haitumiki. Daftari hili linajumuisha takwimu kutoka kote duniani ambazo awali zilikuwa zimetapakaa. [...]

17/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa watoa wito wa maridhiano Sudan Kusini

Kusikiliza / Toby Lanzer akiwa ziarani Sudan Kusini (picha ya maktaba)

Mratibu Mkaazi wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer, ametoa wito kuwepo maridhiano baina ya jamii za taifa hilo ili kutatua mzozo uliopo sasa. Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema hayo kupitia redio ya Umoja wa Mataifa nchini humo, Redio Miraya, wakati wa ziara yake na wawakilishi wa mashirika ya kibinadamu kwenye [...]

17/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban arejelea wito wa amani Ukraine

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anafuatailia kwa makini hali nchini Ukraine tangu kuanza kwa mzozo huo na amezitaka pande kinzani kuepuka kuchukua hatua za haraka wakati huu ambapo vuguvugu la sintofahamu limetawala. Taarifa iliyotolewa leo mjiniNew Yorkna msemaji wa Katibu Mkuu imemkariri Bwana Ban akisema amesikitishwa na rasimu ya jimbo laCrimeaambalo [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu mashuhuri wataka UM kunusuru wakimbizi wa Palestina

Kusikiliza / palestinian-refugees

Waigizaji nguli Emma Thompson na Hugh Grant, kutoka Uingereza ni miongoni mwa watu waliotoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na rais wa baraza kuu la Umoja huo kuandaa maazingira salama na kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada iwafikie waathirika wa machafuko nchini Palestina. Wengine waliotaka hatua zichukuliwe kuwalinda raia hao hususani wakimbizi [...]

17/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujasiriamali waelezwa kuwa muarubaini wa kuwakomboa wanawake kiuchumi

Kusikiliza / Wanawake wa Kimaasai Tanzania

Kujijengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi hususani kujikita katika ujasiriamali ni mbinu mbadala ya kuwakomboa wanawake walioko katika katika maeneo ya pembezoni. Katika mahojiano maalum na idhaa hii, mwakilishi wa kundi la watu asilia, wamasai kutoka nchini Tanzania Grace Mayasek amesema kufuatia mijadala mbalimbali ya kikao cha 58 kuhusu hali ya wanawake kinachoendela mjini New York, [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali Afghanistan kabla ya uchaguzi

Kusikiliza / Ján Kubiš ,Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu UNAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali nchini Afghanistan, ambapo pia limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali nchini humo, ikiwasilishwa na Mwakilishi wake na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMA. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA)  Bwana  Ján Kubiš, ambaye ni Mwakilishi wa Katibu [...]

17/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Korea Kaskazini yaipinga ripoti inayoelezea uvunjifu wa haki za binadamu

Kusikiliza / DPRK commission of inquiry

Korea ya Kaskazini imeipinga vikali ripoti iliyotolewa na kamishna huru iliyochunguza juu ya kufanyika kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadmau na kueleza kwamba ripoti hiyo imejaaa vitu vya kutunga. Mwanadiplomasia wake mjini Geneva So Se Pyong amesema kuwa wale waliotoa ushahidi mbele ya tume hiyo walikuwa ni wasaliti na ambao walikimbia nchi kutokana [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM kuhusu Mynmar awasilisha ripoti yake ya mwisho

Kusikiliza / Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Mynmar Tomás Ojea Quintana

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Mynmar Tomás Ojea Quintana,leo amewasilisha rasmi ripoti yake ya mwisho inayoelezea hali jumla ya haki za binadamu katika kipindi cha miaka 6 kabla ya kumaliza muhula wake baadaye mwaka huu. Mtaalamu huyo ambaye amewasilisha ripoti hiyo mbele ya baraza la haki za binadamu imezitaja hatua zilizopigwa na taifa [...]

17/03/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay kuizuru Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, atafanya ziara ya siku tatu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ili kuzungumzia hali mbaya ya haki za binadamu nchini humo na serikali ya mpito, taasisi muhimu za kimataifa na vikosi vya kulinda usalama. Alice Kariuki na taarifa kamili (TAARIFA YA ALICE) [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR kujenga kambi zaidi kunusuru wakimbizi wa Sudani Kusini

Kusikiliza / Ujenzi wa choo kambini Dadaab nchini Kenya kufuatia ongezeko la wakimbizi kutoka Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linalazimika kuanzisha kambi mpya za wakimbizi kutoka Sudani Kusini wanaoendelea kumiminika nchi jirani wakikimbia macahafuko nchini mwao. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo Adrian Edwards mpango huo utatekelezwa nchini Uganda ,Kenya , na Ethiopia nchi ambazo zimeshuhudia lundo la wakimbizi hao wanaokadiriwa kuwa zaidi [...]

17/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031