Nyumbani » 14/03/2014 Entries posted on “Machi 14th, 2014”

Haikupunguzii chochote kumpa mwanamke nafasi: Mwanamitindo Flaviana Matata

Kusikiliza / Joseph Msami na Falviana Matata katika mahojiano

Wakati mikutano mbalimbali kuhusu hali ya ya wanwake ikiendelea mjini New York Marekani, mwanamitindo nguli wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata ambaye pia anamiliki taasisi iitwayo Flaviana Matata inayotoa misaada ya kielimu, amesema ikiwa wanawake watainuana na kupeana nafasi watapiga hatua kwani kufanya hivyo kunatoa fursa zaidi kwa kundihilo.   Katika mahiojiano maalum na Joseph [...]

14/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa UNSMIL Libya

Kusikiliza / Baraza la Usalama

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Libya, UNSMIL hadi tarehe 13 Machi  2015. Kwa mujibu wa azimio hilo, UNSMIL itaendelea kusaidia katika juhudi za serikali ya mpito za kukaribisha democracia, ikiwemo kupitia kuendeleza na kutoa ushauri wa kitaalam [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la Hakiza Binadamu katika DPRK lizingatiwe haraka: UM

Kusikiliza / Bendera ya DPRK

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu wajibu wa kulinda, Jennifer Welsh, ameelezea kusikitishwa na matokeo ya uchunguzi kuhusu haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, ambayo yaliwekwa bayana mnamo Februari 17, 2014, na ambayo yatawasilishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu. Kutokana na ushahidi uliokusanywa kutoka kwa wataalam, na waathiriwa [...]

14/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kinachoendelea Burundi chamtia hofu Katibu Mkuu wa UM

Kusikiliza / Katibu mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anasikitishwa sana na kile kinachoendelea hivi sasa nchini Burundi hususan ghasia na vurugu za wiki iliyopita kati ya polisi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini humo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Katibu Mkuu akisema kuwa serikali na vyama vya siasa ni lazima [...]

14/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW58 wamulikwa

Kusikiliza / Nembo ya CSW

Mkutano wa 58 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, umeanza mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York. Ajenda kuu ni kuangalia hali ya wanawake na wasichana iko vipi wakati huu ambapo malengo ya maendeleo ya milenia yanafikia ukomo mwakani na nini kifanyike kuhakikisha ajenda baada ya mwaka 2015 inazingatia [...]

14/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Pande kinzani Syria legezeni misimamo yenu kuokoa wananchi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaka pande zinazokinzana nchini Syria ambazo ni Serikali na upinzani kulegeza misimamo yao na kuweka mbele maslahi ya wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa faragha, Ban amesema hata baada ya awamu mbili za mazungumzo ya [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inakabiliana na hali ya kiafya ya wakimbizi walioko Cameroon

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka CAR wanaowasili nchini Camerron

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR imesema wakimbizi wengi wanaokimbia mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawasili Mashariki mwa Cameroon wakiwa na njaa na hata magonjwakamavile Malaria na utapiamlo. (Fatoumata Lejeune-Kaba ni kutoka UNHCR)  "Asilimia 80 ya wanaowasili wana magonjwa kama Malaria, zaidi ya asilimia 20 ya watoto wanaugua utapiamlo tangu [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ombi la misaada ya kibinadamu Syria limefadhiliwa kwa asilimia 9 tu: OCHA

Kusikiliza / Kambi ya kuwahifadhi wakimbizi wa Syria (Picha ya UNHCR)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo linafanya mkutano wa faragha kuhusu hali nchiniSyria, wakati Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, ikisema kuwa kuna uhaba wa ufadhili kwa mashirika yote ya kibinadamu yanayohudumu nchini humo  na katika nchi jirani kuliko wakimbizi. Grace Kaneiya na taarifa kamili (Taarifa ya Grace Kaneiya) Ombi lililotolewa kwa ufadhili [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka vikosi vya usalama kutochochea machafuko Nigeria

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navy Pillay amesema licha ya kwamba ni muhimu serikali ya Nigeria kutuma vikosi vya usalama kutuliza ghasia husuani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo vuguvugu la machafuko yanaoendeshwa na kundi lenye msimamo mkali, Boko Haram, ni muhimu vikosi hivyo visiongeze tatizo kwa matendo yanayosababisha kupoteza makazi, kuhatarisha [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo Sudan Kusini hatarini kuongezeka zaidi: ICRC

Kusikiliza / ICRC yagawa chakula NCHINI Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini, Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu, ICRC imesema mapigano yanayoendelea nchini humo yanasababisha ongezeko la majeruhi na wengine wengi wako hatarini kupoteza maisha kutokana na kukosa matibabu. ICRC inasema tangu kuanza kwa mapigano hayo mwezi Disemba mwaka jana imeshafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 1,200 lakini hali bado ni mbaya na haitabiriki [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Teknolojia kutumika kutokomeza usafirishaji binadamu

Kusikiliza / Nelly Niyonzima  na Joseph Msami wakati wa mahojiano

Matumizi ya teknolojia mathalnai simu za mikononi ni miongoni mwa m,binu stahiki za kufikisha elimu juu ya ukomeshaji wa biashara haramu ya usafirishaji wa bindamu inayoathiri zaidi wanawake na wasichana.  Akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa hali ya wanawake duniani unaondelea mjini New York, Marekani, ulioangazia ukubwa wa biashara hiyo barani Afrika na [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twaomba UM uharakishe jeshi la ulinzi wa amani CAR: Viongozi wa kidini

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akiwa na viongozi wa kidini kutoka CAR. Kutoka kushoto Imam Omar Kobine Layama, Mchungaji Nicolas Guérékoyamé Gbangou na Askofu Mkuu Dieudonné Nzapalainga, baada ya mazungumzo mjini New York, Alhamisi.

  Viongozi wa madhehebu ya kiislamu na kikristo kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wamesihi Umoja wa Mataifa kuchagiza mpango wa kupeleka ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo ili kuepusha kuendelea kuzorota kwa amani nchini humo. Wamesema hayo katika kauli zao mbele ya waandishi wa habari mjini New York baada ya mazungumzo na Katibu [...]

14/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031