Nyumbani » 06/03/2014 Entries posted on “Machi 6th, 2014”

FAO na EU zasaidia wakulima wa Zimbabwe kuongeza uzalishaji wao

Kusikiliza / grains fao

Muungano wa nchi za Ulaya, EU na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na serikali ya Zimbabwe, zimezindua programu ya kina ya kuwasaidia wakulima maskini wanaojishughulisha na uzalishaji mdogomdogo kuoengeza uzalishaji wao. Programu hiyo pia inalenga kuwawezesha kushiriki katika kilimo cha biashara kupitia mbinu jumuishi za ukulima. Programu hiyo ya miaka minne yenye thamani [...]

06/03/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vijana wanajua wanachotaka: Ashe

Kusikiliza / John Ashe

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe amezungumza katika mkutano uliojadili mchango wa wanawake, vijana na asasi za kiraia kuelekea ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015 na kusema vijana kote duniani wanajua wanacghotaka na kuhitaji. Bwana Ashe amesema wakati malengo ya maendeleo ya milenia yakiwa yanaelekea ukomo wake mwak 2015 ikumbukwe [...]

06/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazindua kampeni mpya: 'Watoto sio wanajeshi'

Kusikiliza / Kampeni ya watoto sio wanajeshi

  Kampeni mpya ya kupinga usajili wa watoto katika vita vya silaha imezinduliwa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kampeni hiyo iitwayo, 'Watoto sio Wanajeshi' inaongozwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Watoto katika vita vya silaha, Leila Zerrougui na Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF. Ujumbe wa Katibu [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatudhibiti rasi ya Crimea: Balozi Sergeyev

Kusikiliza / Balozi Yuriy Sergeyev

Mwakilishi wa kudumu waUkrainekwenye Umoja wa  Mataifa Yuriy Sergeyev amesema nchi yake haidhibiti eneo liitwalo Crimea na badala yake Urusi ndiyo inayotawala eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari mjiniNew Yorkmuda mfupi baada ya kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililojadili kuzorota kwa usalama Crimea nchiniUkraine. Balozi  Sergeyev amesema licha ya kwamba [...]

06/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres aelezea kushangazwa na viwango vya ukatili CAR

Kusikiliza / Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kuwa mzozo uliopo sasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati si kitu kilichoibuka upya, kwani taifa hilo limekuwa likikumbwa na matatizo ya aina moja au nyingine kwa muda mrefu. Bwana Guterres amesema hayo akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wainua wanawake Tanzania

Kusikiliza / Chantal Mwang'onda

Dunia ikiwa inaelekea kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Umoja wa Mataifa uko mstari wa mbele kuwawezesha wanawake katika maeneo mbalimbali ikiwamo afya ya uzazi, mazingira na hata kuwajengea uwezo wa kujiamini. Nchini Tanzania Umoja huo kupitia chama cha umoja wa Mataifa cha vijana YUNA umejikita katika kutoa elimu na miongonimwa walionufaika ni Chantal [...]

06/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Hali katika CAR yahitaji hatua za dharura: Valerie Amos

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA, Valerie Amos wakati wa kikao cha Baraza la Usalama

Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, amesema kuwa hali katika Jamhuri ya Afrika tya Kati ni mbaya mno na hatua za dharura zinahitajika ili kuepusha umwagaji damu zaidi. Bi Amos amesema hayo wakati akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuongeza [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake kujumuishwa katika malengo endelevu ya milenia baada ya 2015

Kusikiliza / Phumzile Mlambo Ngcuka

Vita dhidi ya ukatili kwa wanawake utakuwa ni sehemu ya malengo yanayopwa kipaumbele kuelekea malengo ya maendeleo ya milenia baada ya mwaka 2015 amesema mkrugenzi mkuu wa kitengo cha masuakla ya wanawake katika Umoja wa Mataifa Phumzile Mlambo-Ngcuka Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bi Ngcuka amesema suala hili ni mtambuka akitolea mfano [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna fursa ya wanawake kujikwamua licha ya ulemavu

Kusikiliza / disability not inability

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka kuna baadhi ya changamoto amabazo huwakabili wanawake katika jamii. Je hali inakuwajekamamtu ni mwanamke anayeishi na ulemavu Salim Chiro wa radio washirika pwani fm amezungumza na mwanamke mmoja ambaye ameweza kujikwamua licha ya ulemavu

06/03/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Gharama zisiwe kikwazo kuboresha mfumo wa kukusanya takwimu:

Kusikiliza / Dkt Albina Chuwa na Hajjat Amina Mrisho Said

Mkutano wa 45 wa Umoja wa Mataifa kuhusu takwimu unaendelea mjini New York, Marekani ambapo wataalamu wa takwimu kutoka nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea wanajadili mustkhbali wa jukumu la takwimu katika ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 malengo ya maendeleo ya milenia yanapofikia ukomo. Miongoni mwa washiriki ni Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya [...]

06/03/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wanufaisha vijana wa kike Tanzania

Kusikiliza / Girls Tanzania

Tunapoelekea siku ya wanawake duniani March nane, imeelezwa kuwa kupitia chama cha Umoja wa Mataifa cha vijana nchini Tanzania YUNA wanawake wengi wamefunzwa juu ya utunzaji wa mazingira, kilimo pamoja na afya ya uzazi. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Shantal Mwango'nda ambaye ni mmoja wa wanachama wa YUNA ameiambia idhaa hii kuwa vijana hususani [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali katika CAR yamulikwa kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kwa ajili ya hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku wanachama wake wakisikiliza ripoti za hali halisi nchini humo. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali katika CAR, imewasilishwa na Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika [...]

06/03/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo wa huduma za kuzuia mimba

Kusikiliza / contraception Tanzania

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani Machi 8, Shirika la afya duniani WHO limezindua muongozo mpya wa kusaidia nchi kuhakikisha haki za bindadamu zinaheshimiwa wakati wa kutoa huduma za afya ya uzazi kwa wasichana, wanawake na wapenzi kwa kuwapa taarifa zinazohitajika ili kuepukana na mimba zisizotakikana. Alice Kariuki na taarifa kamili TAARIFA YA ALICE Takriban [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Teknolojia ya kisasa kurahisisha ukusanyaji wa takwimu: Tanzania

Kusikiliza / Teknolojia mpya

Wakati mkutano wa 45 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Takwimu unaendelea mjini New York Marekani kuangalia jukumu la takwimu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015,Tanzania imesema wakati umefika kuungana na mataifa mengine katika kutumia teknolojia za kisasa kukusanya takwimu ili kuhakikisha mfumo utumikao unaendana na ule ya kimataifa. Dkt Albina Chuwa anayewakilishaTanzaniakwenye mkutano [...]

06/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula zaongezeka mwezi February : FAO

Kusikiliza / food index

Hali mbaya ya hewa,kuongezeka kwa mahitaji pamoja na usalama ni miongoni mwa sababu za kupanda kwa bei ya chakula kwa mwezi February duniani hususani katika nchi ambazo ni kinara katika uzalishaji wa chakula limesema shirika la chakula nakilimo duniani FAO. Joseph Msami na taarifa kamili (TAARIFA YA MSAMI) Kwa mujibu wa FAO bei za vyakula [...]

06/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Cambodia yapongezwa kwa kufanyia marekebisho ya mfumo wa uchaguzi

Kusikiliza / Ramana ya Cambodia

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia, Surya P. Subedi, amelipongeza taifa hilo kwa makubaliano ya vipengee vitano kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi, ambayo yalifikiwa na vyama viwili vikubwa vya kisiasa bungeni. Amekaribisha pia hatua ya kuondoa marufuku ilowekwa mnamo tarehe 5 Januari 2014 dhidi ya kufanya [...]

06/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930