Nyumbani » 05/03/2014 Entries posted on “Machi 5th, 2014”

Mwanamke ajikwamua kwa kilimo mjini

Kusikiliza / Nyanya

Ikiwa tunaelekea siku chache kabla ya siku ya wanawake duniani kilimo ni kiungo muhimu katika kuchagiza maendeleo na kuhakikisha uhakika wa chakula. Wakati mwingi kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa jamii nyingi barani Afrika hufanyika vijijini lakini hukoMombasa Kenya kuna mwanamke mmoja ambaye anaendehsa kilimo mjini gorofani. Salim Pwani wa Radio washirika Pwani fm [...]

05/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa katika kuteketeza silaha za kemikali Syria: Kaag

Kusikiliza / Sigrid Kaag

Mkuu wa Ujumbe wa pamoja wa kuteketeza silaha za kemikali za Syria, Sigrid Kaag, amesema katika siku chache zilizopita, serikali ya Syria imeongeza kasi ya juhudi za kuteketeza silaha zake za kemikali, na kwamba kuna uwezekano wa kuhitimisha shughuli hiyo ifikapo tarehe ya mwisho ilowekwa ya Juni 30, 2014 ikiwa serikali hiyo itazingatia ratiba yake [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM alazimika kuhitimisha shughuli eneo la Crimea, Ukraine

Kusikiliza / Robert Serry (Picha -Maktaba)

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa aliyekwenda kukagua hali ilivyo katika eneo la Crimea, Ukraine, amelazimika kuhitimisha ghafla shughuli zake katika eneo hilo kwa sababu za kiusalama, kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson. Bwana Eliasson amesema kuwa Bwana Robert Serry, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati, alikutana na watu [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasafiri wahamasishwa kupambana na usafirishaji haramu

Kusikiliza / UNODC_DRUGS

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayojihusisha na utalii, madawa ya kulevya na elimu yamezindua kampeni ya kimataifa ya kupinga aina mbalimbali za usafirishaji haramu. Alice Kariuki na taarifa kamili: (TAARIFA YA ALICE) Mashirika hayo matatu lile linalojihusisha na utalii (UNTWO), ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupinga madawa ya kulevya na uhalifu (UNODC) kwa kushirikiana [...]

05/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yaanza kukusanya maoni ya umma kuhusu kiwango sahihi cha sukari

Kusikiliza / Vyakula ambavyo WHO inasema vinasababisha utipwatipwa na kuoza kwa meno

Shirika la afya duniani, WHO imezindua mpango wake wa kukusanya maoni ya umma juu ya rasimu ya mwongozo wa kiwango sahihi cha sukari kwa binadamu kwa siku. Mwongozo huo ukikamilika utapatia nchi wanachama mwongozo wa jinsi ya kudhibiti matumizi ya sukari kama njia mojawapo ya kupunguza matatizo ya kiafya ikiwemo unene wa kupindukia na matatizo [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikwazo vya silaha Somalia

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza muda wa vikwazo vya silaha nchini Somalia, lakini likaruhusu serikali ya Somalia kununua silaha kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taifa hilo, hadi tarehe 25 Oktoba mwaka huu wa 2014. Azimio hilo limetokana na kufanyiwa marekebisho azimio namba 2093 la tarehe 6 Machi, [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wafunga pazia la ofisi yake ya kisiasa Sierra Leone, UNIPSIL

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Freetown, Jumatano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo ameshuhudia kuhitimishwa kwa jukumu la ofisi ya Umoja huo ya kisiasa na ujenzi wa amani Sierra Leone, UNIPSIL na kuelezea shukrani zake kwa ushirikiano uliotolewa na wananchi na serikali wakati wa kipindi chote cha zaidi ya miaka 15 ya operesheni za ofisi hiyo na zilizotangulia. Taarifa [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujasiri wamwezesha Isca kujikita katika biashara iliyotawaliwa zaidi na wanaume

Kusikiliza / Isca Kauga-Joshua

Kauli ya Umoja wa Mataifa ya kwamba usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote imethibitika kwa mtanzania Isca Kauga-Joshua aishie Marekani aliyeamua kuvunja mipaka ya biashara ya upigaji picha za mnato na video iliyotawaliwa zaidi na wanaume ambayo sasa amesema imemwezesha kuboresha maisha yake na familia yake. Akizungumza katika mahojiano maalum na mdau mshirika wa [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasyria wanakabiliwa na hali ngumu na njaa

Kusikiliza / Wasyria wanokimbia mapigano kuelekea nchi jirani

Mamia ya wananchi wa Syria wanaripotiwa kuwa katika hali mbaya wengi wao wakiwa wamelundikana kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na mabomu hali ambayo inazidisha wasiwasi mkubwa.  Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti moja iliyotolewa na Kamishana moja ya. Taarifa kamili na George Njogopa. (Taarifa ya george) Ripoti hiyo inasema kuwa  wamekuwa na mbinu za makusudi zinazofanywa ili [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO alaani vikali mauaji ya mwandishi Colombia

Kusikiliza / Kamera ya mwanahabari

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova, amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa mwandishi wa habari Yonni Steven Caicedo  nchini Colombia aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana hapo February 19. Mwandishi huyo ambaye amekuwa akifanya kazi na kituo kimoja cha televisheni kama mpiga picha amekuwa akiishi maisha ya kujificha ficha kwa kipindi kirefu kufuatia vitisho alivyokuwa akivipata kuhusu [...]

05/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nchi kusaidiwa kufikia malengo ya uchumi unaojali mazingira

Kusikiliza / Mazingira

Kumekuwa na mikakati ya kuziwezesha nchi ziweze kufikia shabaha ya kuendesha uchumi unaojali mazingira  ifikapo mwaka 2020.   Mipango hiyo ni pamoja na kuziwezesha nchi kuzingatia sera ambazo zitatilia mkazo utekelezaji wa miradi endelevu. Nchi ambazo zinatazamiwa kupigwa jeki ni pamoja na Burkina Faso, Peru, Mauritius, Mongolia,na Senegal.   Ili kufanikisha mkakati nchi wahisani zimetangaza [...]

05/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031