Nyumbani » 04/03/2014 Entries posted on “Machi 4th, 2014”

Ban apigia debe kilimo cha kaya kwa maendeleo vijijini

Kusikiliza / wakulima wa kaya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa serikali ziwawezeshe wakulima wa kaya kwa kubuni sera zinazoweka mazingira stahiki kwa usawa na maendeleo endelevu vijijin, katika kuendeleza ujumbe wa 2014 ambao umetengazwa kuwa Mwaka wa Kilimo cha Kaya. Hayo ni katika ujumbe wake kwa kongamano na maonyesho ya kimataifa kuhusu kilimo cha [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Eliasson akutana na Kaimu Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine: Serry awasili Crimea

Kusikiliza / Mabaki ya magari yaliyochomwa moto kutokana na maandamano  ya hivi karibuni huko Kiev, Ukraine. (Picha-Umoja wa Mataifa)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ambaye yuko nchii Ukraine hii leo amekuwa na mazungumzo na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Andrii Deshchytsia, mjini Keiv ambako wamejadili mzozo unaoendelea nchini humo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema wawili hao wamesisitiza umuhimu wa utulivu na mshikamano wa [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya kuboresha miji duniani yazinduliwa hii leo:

Kusikiliza / Jiji tutakalo

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi ya watu, UN-HABITAT na wadau wake leo limezindua kijitabu ambacho ni dira ya aina ya miji inayotakiwa katika karne ya 21. Uzinduzi wa kijitabu hicho umefanyika New York ikiwa ni sehemu ya kampni ya ushirikiano duniani ya kuboresha miji kuelekea mkutano wa saba wa majiji utakaofanyika huko Colombia [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OPCW yapokea pendekezo la Syria kuhusu uondoshaji wa kemikali nje ya nchi hiyo

Kusikiliza / OPCW

Serikali ya Syria imewasilisha pendekezo jipya lenye lengo la kuhakikisha uondoshaji wa kemikali zenye sumu nje ya nchi hiyo unakamilika kabla ya mwisho wa mwezi ujao wa Aprili. Shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW limepokea pendekezo hilo likiitaka Syria kuhakikisha linazingatia muda kwani awali kemikali hizo za sumu zilitakiwa ziwe zimeshaondolewa nchini [...]

04/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake Tanzania wainua vipato vyao kwa kutumia teknolojia

Kusikiliza / Ufugaji wa kuku

Wanawake nchini Tanzania wanasema kwa kutumia teknolojia wamefanikiwa kuinua vipato vyao katika ujasiriamali na hivyo kuwasaidia katika kuinua uchumi wa familia na jamii nzima kwa ujumla.  Wamemweleza Penina Kajura wa radio washrika Afya radio ya Mwanza nchini humo kuwa ustawi wa biashara zao unategemea zaidi mitandao ya kijamii na hata teknolojia za simu ikiwa ni [...]

04/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za wahamiaji zamulikwa Geneva

Kusikiliza / Jan Eliasson

Mkutano wa 25 wa baraza la haki za binadamu unaoendelea mjini Geneva leo umejikita kwenye haki za wahamiaji ambapo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ametoa ujumbe wa video kuhusu haki za binadamu akisema ni muhimu changamoto zinzokabili kundi hilo zikatatuliwa na serikali pamoja na jamii kwa ujumla. (SAUTI ELIASSON)

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya Sudan Kusini yanakwamisha misaada kwa watoto

Kusikiliza / Wakimbizi hawa wa Sudan Kusini wanahitaji misaada muhimu ya kujikimu. (Picha: UNHCR)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema mapigano mapya huko Sudan Kusini yanakwamisha jitihada zake za kupeleka misaada kwa watoto. Msemaji wa shirika hilo mjini Geneva, Uswisi, Patrick Mccormick amesema mamia ya maelfu ya wanawake, wanauame na watoto hawawezi kufikiwa ili kupatiwa misaada ya dharura ikiwemo maji safi na salama na huduma [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IFRC na UNAIDS walenga kuwatibu watu milioni 15 waishio na HIV ifikapo 2015

Kusikiliza / UNAIDS

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu na Shirika la Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu HIV na Ukimwi, UNAIDS, yamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuendeleza juhudi za kuongeza upimaji na matibabu dhidi ya virusi vya HIV. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) Kwa mujibu wa makubaliano hayo, IFRC [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake watakiwa kutumia uhuru na mitaji kujikwamua kiuchumi

Kusikiliza / Alice Kabatoro

Mitaji midogo nauhuru walionao wanawake ni sehemu ya nyenzo muhimu ambazo ikiwa watazitumia zinaweza kuwainua kiuchumi na hata kijamii, amesema mmoja wa wanawake wafanyabiashra wakubw anchini Uganda Katika mahojiano na John Kibego wa radio washirika Spice Fm ya nchini Uganda mfanyabiashara huyo Alice Kabatoro anayemiliki mgahawa na nyumba ya wageni huko Hoima, amesema licha ya [...]

04/03/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuchochea mabadiliko kufanyike kwa vitendo: Kongamano

Kusikiliza / Mwanamke mkulima

Katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani, Machi Nane mjini New York kumefanyika mkutano wenye lengo la kuchochea mabadiliko ya wanawake kwa vitendo hususan katika sekta binafsi. Kongamano hilo linatathmini mabadiliko dhahiri kwa wanawake ndani ya miaka 20 na changamoto wanazokabiliana nazo. Wakati hayo yakiendelea nchini Kenya Mtaalamu wa kilimo huko Mombasa Pauline Ndiso [...]

04/03/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulio nchini Bahrain

Kusikiliza / Ramana ya Bahrain

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatatu kwenye kijiji cha Daih nchini Bahrain kilichosababisha vifo vya polisi watatu. Katika taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban amekaririwa akituma rambirambi kwa familia za wafiwa na kwa serikali ya Bahrain huku akisema vitendo kama hivyo haviwezi kuhalalishwa kwa sababu [...]

04/03/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yasambaza msaada muhimu wa chakula huko Mashariki mwa DRC

Kusikiliza / Mgao wa chakula nchini DRC

Shirika la Mpango wa chakula duniani, WFP limeanza kusambaza mgao wa vyakula kwa watu 74,000 walioathiriwa na mzozo wa mapigano kwenye eneo la Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakazi wa eneo hilo lililo mpakani mwa Uganda wamekuwa wakirejea baada ya eneo hilo kushambuliwa na kushikiliwa na waasi miezi sita ya mwisho [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka usaidizi kwa wakimbizi wa CAR na Sudan Kusini uharakishwe

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika

Zaidi ya watu Milioni Moja na Laki Nane wamekimbia makazi yao huko Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na majanga yanayoendelea kwenye nchi zao, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR katika kile kinachoelezwa kuwa ni kiwango kikubwa zaidi cha ukimbizi barani Afrika katika miaka ya karibuni. Tupate taarifa. [...]

04/03/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930