Valerie Amos asikitishwa na kuanza tena mapigano Homs, Syria

Kusikiliza /

Valerie Amos, Mkuu wa OCHA

Mratibu mkuu wa shughuli za kibinadamu na masuala ya dharura katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ameelezea kusikitishwa kwake na kuvunwja kwa makubaliano ya kusikitishwa mapigano kwa siku tatu yalofikiwa na pande zinazozozana nchini Syria ili huduma za kibinadamu zifikishiwe raia. Bi Amos pia amefadhaishwa na kulengwa makusudi kwa wahudumu wa kibinadamu katika mapigano hayo.

Afisa huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amewapelekea risala za pole watu walojeruhiwa katika mapigano hayo, na kusifia ujasiri na kutokata tamaa kwa mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na wahudumu wengine wa Umoja wa Mataifa pamoja na wale wa Hilali Nyekundu ambao waliingia kwenye mji wa Homs ili kujaribu kuwafikishia raia misaada ya dharura.

Bi Amos pia amesema matukio hayo yamedhihirisha tena hatari wanazokumbana nazo raia na wahudumu wa kibinadamu kila siku kote nchini Syria, na kutoa wito kwa wale wanaopigana waheshimu usitishaji mapigano kwa sababu za kibinadamu, kuhakikisha raia wanalindwa na kuwezesha kuwafikishia misaada. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu hawatovunjwa moyo, na wataendelea kufanya kila liwezekanalo ili kuwafikishia misaada wale wanaoihitaji.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031