Umoja wa Mataifa washindwa tena kugawa misaada ya dharura kwenye kambi ya Yarmouk, Syria

Kusikiliza /

 

kambi ya yarmouk mjini Damascus

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limesema kuwa hii leo limeshindwa tena kugawa misaada ya chakula na vifaa vingine vya kibinadamu katika kambi ya Yarmouk, iliyoko Damascus.

Msemaji wa UNRWA, Chris Gunness, amesema kuwa UNRWA haijaweza kugawa chakula katika kambi hiyo kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa, hali ambayo inayahatarisha maisha ya raia ambao wamenaswa katika mzozo wa Syria , na ambao wanategemea UNRWA kupata chakula na vifaa vyote vya matibabu.

Ameongeza kuwa UNRWA imeweza kugawa vifurushi 6,500 vya chakula tangu January 18. Hata hivyo, amesema kapu moja la chakula hutumiwa tu kwa muda wa siku 10 na familia kwa wastani, na hivyo vile walivyogawa vitakuwa vimekwisha sasa. Ameongeza kuwa kwa sababu ya kuwepo hali mbaya, kama vile utapia mlo kuripotiwa kuongezeka, hatma ya wanawake na watoto hasa inaendelea kutia hofu.

UNRWA imesema Umoja wa Mataifa ni lazima uwe na uwezo wa kusambaza misaada ya kibinadamu kwa raia hao wanaoteseka kutokana na kuzingirwa katika kambi hiyo ya Yarmouk, kwa njia salama na kwa njia endelevu.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930