Ukata wakabili mpango wa UNDP kuondoa mabomu ya ardhini Cambodia

Kusikiliza /

(UNDP/Chansok Lay)

Shirika la mpango wa maendeleo la UM (UNDP) limeelezea wasiwasi wake juu ya upungufu wa wahisani wa kusaidia mpango wa kuondoa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Cambodia. Nchi hiyo imeathirika kutokana na mabaki ya mabomu hayo baada ya miaka 30 ya vita uliomalizika katika miaka ya tisini.

Ingawa utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa karibu kilomita 2000 za ardhi nchini zimechafuliwa na mabomu ya kutegwa, kiasi kamili cha uchafuzi huo hakijulikani. Kazi ya kusafisha mabomu imekuwa ikiendelea kwa miongo miwili lakini bado kuna kazi nyingi ya kufanya.

Bi Tong Try, ni afisa wa UNDP Cambodia.

Hatujaweza kuondoa mabomu yote ya kutegwa ardhini nchini Cambodia kwa sababu ya ukosefu wa fedha, hivyo tunahitaji kushughulikia masuala muhimu kwanza. Tunatumia mchakato wa ndani wa kuangalia ni maeneo gani yanayohitaji kusafishwa, kwanza kupunguza hatari ya majeruhi na pili kuharakisha uwezekano wa mapato ya watu na uchumi endelevu wa nchi.

UNDP ni miongoni mwa wadau wengi ambao wanatoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa ajili ya mpango wa kusafisha mabomu Cambodia.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031