Saratani haitaondoka kwa kutegemea tiba pekee-Ripoti

Kusikiliza /

Mojawapo ya vituo vya uchunguzi wa saratani nchini Nigeria

Ripoti moja imeonya leo kwamba juhudi za kukabiliana na tatizo la saratani duniani haziwezi kuzaa matunda kwa kuendelea kutegemea matibabu pekee bila kuchukua hatua ya kuzuia kasi ya ugonjwa huo.  Ripoti hiyo iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya saratani imehimiza juu ya kutolewa kwa kinga dhidi ya magonjwa kamaini. Grace Kaneiya na maelezo zaidi

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Kulingana na ripoti hiyo mpya , maeneo yanayopaswa kuzingatiwa ni pamoja na kuweka jitihada kuzuia kuenea kwa matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku hasa katika nchi zile zenye kipato cha chini na kile cha kati.

Pia ripoti hiyo imezitaka nchi zilizoendelea kiviwanda kuwahimiza wananchi wake kushiriki mazoezi ya viungo ya mara kwa mara.

Akielezea kwa ndani juu ya ripoti hiyo,Dk Bernard W. Stewart ambaye ni mmoja wa waliohariri ripoti hiyo, ametaka kuwepo kwa utashi wa kisiasa ili kutekeleza mipango yenye nia ya kuzua matatizo yaletayo saratani.

(Sauti ya Dkt. Benard)

Amesema kuwa viongozi duniani wanapaswa kuanzisha kile kinachojulikana " upimaji na utoaji tiba" ili kupunguza uwezekano wa kujitokeza magonjwa ya saratani.

Mpango umekuwa ukitekelezwa katika nchi zaIndianaCosta Rica, na kuleta mafanikio makubwa

Nchini Tanzania Mariam Zakaria Mkazi wa Ilemela, mkoani Mwanza anasema kilichomsibu kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kubaini anaugua saratani.

(Sauti ya Mariam)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031