OCHA na serikali ya DRC leo kuzindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu

Kusikiliza /

Baada ya amani kurejea Mashariki mwa DRC, wanawake wana matarajio makubwa ya ustawi

Shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi wa kibinadamu, OCHA kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo Alhamisi wanazindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu nchini humo.

Mwandishi wa Radio Okapi Jean-Pierre Elali Ikoko amemkariri Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko DRC kwa masuala ya usaizidi wa binadamu Moustapha Soumaré akisema kuwa mpango huo unaanzishwa wakati huu ambapo makundi yenye silaha yakijisalimisha pamoja na kusambaratishwa kwa waasi wa M23.

(Sauti ya Moustapha)

Kwa mujibu wa Soumaré mpango huo unakuja wakati ule wa mwaka 2013 ukiwa umetimizwa kwa dola Milioni 730 kati ya dola Milioni 892 zilizoombwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930