MONUSCO yaonya makundi ya silaha dhidi ya kuwashambulia wahudumu wake

Kusikiliza /

Walinda amani wapiga doria DRC

Makundi yenye silaha katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, yameonywa kuhusu kufanya mashambulizi dhidi ya  wahudumu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO. Onyo hilo limetolewa na Jemedari Abdallah Wafy, ambaye ni Naibu Mwakilishi maalum wa katibu mkuu na Mkuu wa MONUSCO, ambaye pia ndiye msimamizi wa idara ya utawala wa sheria katika MONUSCO.

Amesema hayo akiwa kwenye mji wa Beni, jimboni Kivu ya Kaskazini, mara tu alipowasili huko saa chache baada ya kuuawa kwa raia mmoja wa Kongo mtumishi wa Monusco hapo Beni.

Bwana Wafy, amesema Monusco itafanya uchunguzi dhidi ya mauaji hayo, hadi kuwawajibisha waliotenda maovu hayo, onyo lililonaswa na mwandishi wa Redio Washirika, Okapi huko Beni, Martial Papy Mukeba.

(SAUTI YA WAFY)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930