Mkuu wa masuala ya kisiasa wa UM ahitimisha ziara nchini Afghanistan

Kusikiliza /

Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman amekamilisha ziara ya siku mbili nchini Afghanistan hii leo, ambayo imekuwa ziara yake ya kwanza nchini humo tangu alipochukuwa wadhfa wa kusimamia masuala ya kisiasa mnamo Julai 2, 2012.

Katika ziara hiyo, Bwana Feltman amejikita katika kupata uelewa wa majukumu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Afghanistan, UNAMA, pamoja na masuala mengine ya usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa taifa la Afghanistan na watu wake.

Pamoja na hayo, amefanya pia mikutano na maafisa wa tume huru ya uchaguzi, IEC, ile ya malalamishi ya uchaguzi, IECC na tume huru ya haki za binadamu, pamoja na maafisa wa kidiplomasia walioko mjini Kabul.

Katika mikutano hiyo, wamejadili masuala kadha wa kadha yanayohusiana na usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan katika uchaguzi, wakati taifa hilo linapokuwa katika harakati za mpito wa kisiasa na kiusalama. Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwa mshirika wa karibu, wa kutegemewa na wa kweli kwa taifa hilo.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930