Mjumbe maalum wa UM yuko DRC kuchagiza mchakato wa amani

Kusikiliza /

Bi. Mary Robinson akiwa katika sehemu ya ziara yake huko DRC. (Picha-MONUSCO)

Mazungumzo kati ya Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye nchi za maziwa makuu Bi. Mary Robinson na viongozi wa serikali huko Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongokuhusu utekelezaji wa mpango wa amani, ulinzi na ushirikiano uliotiwa saini mwezi Februari mwaka jana yamekuwa na manufaa.

Amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa mjiniNew Yorkalipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa katika mazungumzo hayo Bi. Robinson anatoa wito kwa serikali kutimiza ahadi zake za kuleta amani ya kudumu wakati huu ambapo ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo unajiandaa kutembelea eneo la Nyamaboko, Kivu Kaskazini kunakodaiwa kufanyika mauaji ya watu zaidi ya 70.

Tayari Bi. Robinson amekuwa na mazungumzo na Rais Joseph Kabila na maafisa wengine wa serikali kuhusu utekelezaji wa mpango huo  na manufaa yaliyojitokeza katika ngazi ya kitaifa ni pamoja na kuongeza kasi ya marekebisho ya sekta ya ulinzi nchini humo kwa lengo la kupanua wigo wa mamlaka za ulinzi wa kitaifa.

Mjumbe huyo pia amekuwa na mazungumzo na makundi ya kiraia pamoja na wadau wa kimataifa ili kuhamasisha usaidizi wao kwenye mchakato wa amani

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031