Kumbukizi ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari Rwanda yafanyika Umoja wa Mataifa

Kusikiliza /

Kumbukizi hiyo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ilienda sanjari na uwashaji mishumaa

Tunaungana kudhihirishia ulimwengu kuwa tunapinga tofauti zisizo za kiasili zilizowekwa na wakoloni na kutuletea madhara, ni kauli ya Mwakilishi wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Eugene-Richard Gasana, wakati wa kumbukizi ya miaka 20 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Kwibuka20, ambayo mwaka huu dhima yake ni Kumbuka, Ungana na badilika!

Balozi Gasana amesema wanaugana pia kupinga madhila ya utawala usio bora uliotumbukiza nchi yao kwenye janga na juu ya yote..

(Balozi Gasana)

Tunaungana kwasababu tumengaza kuwa kamwe tena kwa wakati wangu! Tunaugana kubadili historia yenye giza ya historia yetu na kuweka majaliwa yenye nuru kwa kizazi kijacho!Tunaungana kurejesha utu wetu na kujenga!
Naye Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe amesema kumbukizi hiyo inatoa fursa ya kuona vile ambavyo Jumuiya ya Kimataifa ilishindwa kuchukua hatua dhidi ya mauaji hayo na amerejelea azma ya kwamba ukiukwaji huo wa utu wa binadamu kamwe hautarudiwa tena.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930