Kikao cha utatu cha UNAMID chatiwa hofu na kuchelewa kwa askari na vifaa

Kusikiliza /

Askari walinda amani wa UNAMID

Hofu juu ya kuchelewa kupelekwa kwa askari na vifaa kwa ajili ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa AFrika, UNAMID huko Darfur, Sudan Kusini imeibuka wakati wa mazungumzo ya kikao hicho mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kikao hicho kikijumuisha wawakilishi kutoka Serikali ya Sudan, AU, na Umoja wa Mataifa kimekubaliana kuwa Sudan ishirikiane na UNAMID kuharakisha kukamilishwa kwa mpango huo haraka iwezekanavyo ili kuepuka mazingira yanayoweza kukwamisha operesheni huko Darfur.

Ajenda nyingine zilikuwa ukosefu wa uhuru wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa watendaji wa UNAMID pamoja na kuzorota kwa usalama hususan mwaka 2013 kutokana na mizozo ya kikabila.

Hata hivyo washiriki walikaribisha ushirikiano kati ya serikali ya Sudan na UNAMID katika ngazi ya ushirikiano wa kiufundi uliosababisha kuondoa mkwamo wa masuala kama ya vibali vya kuingia nchini humo, masuala ya forodha na ukodishaji wa ardhi.

Akizungumzia mkutano huo, Mkuu wa UNAMID Mohammed Ibn Chambas amesema vikao vya aina hiyo vinaimarisha ushirikiano na kurahisisha utendaji kazi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031