Naibu mwakilishi wa UM na nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria athibitisha kuiacha nafasi hiyo

Kusikiliza /

Nasser Al-Kidwa

Naibu mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria, Nasser al-Kidwa amemthibitishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon nia yake ya kuiacha nafasi hiyo ya uwakilishi na kueleza kuwa yuko tayari kuutumikia Umoja huo kwa nafasi yeyote kadri  Katibu Mkuu atakavyoona ni sawa.

Bwana Ban amemshukuru Bwana al-Kidwa kwa utumishi wake chini ya wawakilishi wa Lakdhar Brahimi pamoja na Kofi Annan katika kujaribu kukomesha umwagaji damu nchini Syria na kusongesha mbele utawala wa mpito wa Syria kulingana na makubaliano ya amani ya Geneva mnamo 30 June 2012.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930