Hali ya huduma ya afya imeimarika Afrika Magharibi:UNFPA

Kusikiliza /

Mama akichunguzwa afya yake kwenye moja ya vituo vya afya ya mama na mtoto nchini Sierra Leone. (Picha-UNFPA)

Matokeo ya awali yaliyotolewa wiki hii kuhusiana hali za kaya na afya nchini Sierra Leone yanaonyesha kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa kwa kuboresha mifumo ya utoaji huduma za kiafya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Ripoti hiyo ya matokeo inasema kuwa kwa kulinganisha na tafiti zilizopita taifa hilo limefanikiwa kuboresha huduma zake hasa katika maeneo yanayohusu afya za uzazi.

Kutokana na hali hiyo ripoti inasema kuwa kuna matumaini makubwa kwa Siera Leone kufikia malengo ya maendeleo ya kimataifa.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu duniani UNFPA, mafanikio hayo yaliyoanza kujitokeza ni utambulisho tosha kwamba serikali kwa kushirikiana na mashirika hisani yanafanya kazi.

UNFPA imepongeza utendaji kazi wa Rais Ernest Bai Koroma ambaye katika miaka ya hivi karibuni alianzisha sera ya utoaji matibabu bure kwa kina mama na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031