Dujarric awa msemaji mpya wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza /

Stéphane Dujarric

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemteua Stéphane Dujarric kuwa msemaji mpya wa Umoja wa Mataifa akichukua nafasi ya Martin Nesirky ambaye ameamua kuachia nafasi hiyo na kuwa karibu na familia yake hukoVienna, Austria ambako hata hivyo ataendelea na kazi ndani ya Umoja huo.

Akitangaza uteuzi huo mbele ya waandishi wa habari hii leo, Bwana Ban amesema Dujarric ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari ndani ya Umoja wa Mataifa  ataanza jukumu hilo jipya tarehe 10 mwezi ujao .

Bwana Ban amemwelezea kuwa Bwana Nesirky kuwa ni mtu ambaye amekuwa wazi wakati wote wa kipindi chake cha miaka minne.

(Sauti ya Ban)

Ninashukrani nyingi sana kwa Martin Nesirky kwa bidii yake ya kazi na huduma yake ya kipekee, ushauri wake muhimu na urafiki. Wakati mwingine alizungumza nami bila woga akinishauri jambo, ambapo kila mara nilikubali na mwishowe kila wakati inakuwa ni jambo sahihi. Na ninashukuru sana."

Halikadhalika Bwana Ban amemteua Farhan Haq kuwa Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa nafasi ambayo alikuwa akikaimu huku akisema kuwa ni matumaini yake Dujarric na Farhan watapatiwa ushirikiano wa kutosha ili kutekeleza jukumu hilo.

Akizungumza baada ya tangazo hilo, Nesirky amesema haukuwa uamuzi rahisi lakini anaamini kuwa ni uamuzi sahihi.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2014
T N T K J M P
« nov    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031