Ban, Baraza la Usalama washutumu shambulio huko Lebanon

Baraza la Usalama

Umoja wa Mataifa umeshutumu vikali shambulio lililotokea huko Hermel, Kaskazini-Mashariki mwa Lebanon na kusababisha vifo na majeruhi.

Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ametuma rambirambi zake kwa wafiwa na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi huku akisema ni matumaini yake kuwa wahusika wa tukio hilo la kigaidi watasakwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Amesema tukio hilo la Jumamosi ni mwendelezo wa ugaidi na ghasia nchini Lebanon na linatia wasiwasi.

Bwana Ban amerejelea wito wake kwa wananchi wa Lebanon kuunga mkono jitihada za taasisi za dola ikiwemo vyombo vya usalama kupinga vitendo vya namna hiyo ambapo amesema havikubaliki.

Nalo Baraza la Usalama limeshutumu shambulio hilo ambapo pamoja na kutuma rambirambi limesema ugaidi wa aina yoyote ule haukubaliki. Wajumbe wa baraza hilo wamerejelea taarifa ya wa baraza ya tarehe 10 Julai 2013 inayotaka wananchi kulinda umoja na kuepuka kujihusisha na mzozo wa Syria kwa mujibu wa azimio la Baabda.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930