Ban atoa heko kwa Lebanon kwa kuunda serikali mpya

Kusikiliza /

Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha tangazo la kuundwa kwa serikali mpya nchini Lebanon leo, na kumpa heko Waziri Mkuu Tamam Salam kwa hatua hiyo muhimu.

Taarifa ilotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amewahimiza viongozi wa kisiasa wa Lebanon kuendeleza mazungumzo ya kujenga yalochangia kuundwa kwa serikali hiyo mpya, na kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao wa urais unaendeshwa vyema katika msingi ilowekwa kisheria.

Bwana Ban amempongeza Waziri Mkuu anayeondoka, Najib Mikati kwa uongozi wake, na kusema kuwa Umoja wa Mataifa unatazamia kufanya kazi pamoja na serikali mpya katika juhudi zake za kuwahudumia watu wa Lebanon na kuhakikisha utekelezaji kikamilifu wa azimio namba 1701 la Baraza la Usalama na mengineyo ambayo bado ni muhimu kwa utulivu wa taifa hilo.

Kutokana na ukubwa wa changamoto za kiusalama, kibinadamu na kiuchumi, Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa serikali kuweza kuchukuwa hatua mara moja kukabiliana na changamoto hizo bila kuchelewa, ikiungwa mkono na pande zote.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031