Ban ataka kusitishwa kwa ghasia Venezuela

 

Ramana ya Venezuela

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake na ghasia na upotevu wa maisha kufuatia maandamano ya nchini Venezuela na kutaka juhudi zichukuliwe haraka kupunguza uhasama na kuzuia vurugu zaidi.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu inasema Bwana Ban ameongea na rais wa nchi hiyo na baadhi ya wanavezuela. Bwana Ban amesema anamatumaini pande kinzani zitaondoa tofauti zao na kuandaa mazingira kwa ajili ya majadiliano yenye tija ili amani irejee haraka iwezekanavyo.

Katibu Mkuu ametaka kulindw kwa haki za binadamu kwa raia wote nchini Venezuela . Amewataka raia kutotoa kipaumbele kwenye tofauti zao na kuelezea mahitaji yao kwa njia ya amani kulingana na sheria, na kutafuta usawa.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031