Nyumbani » 27/02/2014 Entries posted on “Febuari 27th, 2014”

Baraza la Usalama lalaani shambulio Somalia

Baraza la Usalama

Shambulio lingine la kigaidi limefanyika hii leo kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kadhaa ambapo wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametoa taarifa kushutumu kitendo hicho na vinginevyo vya aina hiyo. Tayari kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda kimekiri kuhusika nalo huku wajumbe hao wa [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumbukizi ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari Rwanda yafanyika Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Kumbukizi hiyo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ilienda sanjari na uwashaji mishumaa

Tunaungana kudhihirishia ulimwengu kuwa tunapinga tofauti zisizo za kiasili zilizowekwa na wakoloni na kutuletea madhara, ni kauli ya Mwakilishi wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Eugene-Richard Gasana, wakati wa kumbukizi ya miaka 20 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Kwibuka20, ambayo mwaka huu dhima yake ni Kumbuka, Ungana na badilika! Balozi Gasana [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka DRC kuheshimu wajibu wake kwa mujibu wa mkataba wa Roma

Kusikiliza / ICC

Rais wa Baraza la nchi wanachama wa mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Tiina Intelmann, ameitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuheshimu mkataba wa Roma ambao nchi hiyo ni mwanachama. Ametoa wito huo akizingatia kuwa Rais Omar Bashir wa Sudan yuko nchini humo kushiriki mkutano wa kikanda ihali ICC imempatia [...]

27/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mauritania badili ahadi kuwa vitendo ili kudhibiti utumwa: Mtaalamu

Kusikiliza / Gulnara Shahinian

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utumwa Gulnara Shahinian amepongeza Mauritania kwa hatua ilizochukua kutokomeza utumwa nchini humo lakini akataka vitendo zaidi kwa kutekeleza sheria na sera. Amesema hayo mwishoni mwa ziara yake rasmi nchini humo ya kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya awali ambapo ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na mpango wa kuanzisha [...]

27/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Onyesho la filamu ya miaka 12 utumwani yafungua maadhimisho ya biashara ya utumwa atlantiki

Kusikiliza / Utumwa

Maadhimisho ya siku ya utumwa na biashara ya utumwa huadhimishwa kila mwaka Machi 25. Katika kuanza kumbukumbu ya maadhimisho ya mwaka huu yalifunguliwa rasmi na onyesho la filamu Miaka 12 utumwani ambayo mmoja wa waigizaji ni Lupita Nyon’go kutoka Kenya. Onyesho hilo lilifanyika jioni ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na Grace [...]

27/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua kubwa imepigwa Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan: OCHA

Kusikiliza / Watoto nchini Ufilipino

Tacloban ya leo ina tofauti kubwa na ile niliyoshuhudia mwezi Novemba wakati wa ziara yangu ya pili mwezi Novemba mwaka jana, amesema Mkuu wa shirika la misaada ya kiutu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA,  Valerie Amos alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara yake nchini humo Alhamisi. Ripoti ya Flora Nducha inafafanua zaidi.  (Ripoti [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaendelea kuwanusuru wakimbizi Sudani Kusini

Kusikiliza / iom ssudanese relocation

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaendela na opreshenai za kuwanusuru wakimbizi wanaotafuta hifadhi kufuatuia machafuko nchini Sudani Kusini ambapo kwa kutumi usafiri wa boti na basi imewasafirisha wahamiaji 425 kutoka kambi iitwayo Gambella na kuwapeleka nchini Ethiopia IOM pia kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa inasaidia katik akuhamisha vifaa vya mahitaji [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa amani waathiri amani Afrika na Mashariki ya Kati

Kusikiliza / José Graziano da Silva

Hali mbaya ya ukosefu wa chakula nchi za Afrika Kaskazini na baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati sio tu kwamba inasababishwa na vikwazo vya miundo msingi ambavyo ukanda huo unakabiliana navyo katika kuzalisha chakula cha kutosha, kuongezeka kwa utegemezi katika kuagiza chakula lakini pia migogoro, na kuongezeka kwa wakimbizi na wahamiaji amesema mkurugenzi wa [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya mtoto ya kucheza yatimia huko Libya

Kusikiliza / Kituo hiki kilichofunguliwa kimeleta matumaini na furaha kwa watoto na hata wazazi. (Picha-Unicef)

Nchini Libya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali limefungua kituo cha kwanza kati ya 13 vya michezo ya watoto na hivyo kuweka mazingira rafiki na salama kwa kundi hilo kutimiza moja ya haki yao ya msingi ya kucheza kama sehemu muhimu ya kuimarisha makuzi yao. UNICEF inasema hatua [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani kitendo cha gazeti moja Uganda kuweka hadharani majina ya wanaodaiwa kuwa mashoga

Kusikiliza / haki

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali kitendo cha gazeti moja nchini Uganda kuchapisha majina na picha za watu wanaodaiwa kuw ani mashoga na kusema kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya faragha. Msemaji wa Ofisi hiyo Cécile Pouilly amesema kitendo hicho kinadhihirisha hatari dhahiri dhidi ya kundi hilo [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi wa aina yoyote wafanyika leo

Kusikiliza / Kipepeo ndio nembo itumikayo kupinga ubaguzi wa aina yoyote

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza mapambano dhidi ya Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé ameshiriki uzinduzi wa harakati za kuelekea kilele cha siku ya kimataifa ya kupinga aina zote za ubaguzi Machi Mosi. Siku hii inalenga kutoa wito kwa watu popote pale walipo kuendeleza na kutambua haki ya kila mmoja kuishi maisha yenye [...]

27/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031