Nyumbani » 26/02/2014 Entries posted on “Febuari 26th, 2014”

Asilimia 95 ya wapiga kura wamejiandikisha Guinea-Bissau

Kusikiliza / José Ramos-Horta akihutubia baraza la usalama kwa njia ya video kutoka Guinea-Bissau

Wakati Guinea-Bissau ikijiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na wabunge mwezi Aprili mwaka huu, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo José Ramos-Horta amesema takribani asilimia 95 ya watu wanaostahili kupiga kura wamejiandikisha. Bwana Ramos-Horta ameliambia Baraza la Usalama hii leo kuwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Urais kuna wagombea [...]

26/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ataka kusitishwa kwa ghasia Venezuela

Ramana ya Venezuela

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake na ghasia na upotevu wa maisha kufuatia maandamano ya nchini Venezuela na kutaka juhudi zichukuliwe haraka kupunguza uhasama na kuzuia vurugu zaidi. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu inasema Bwana Ban ameongea na rais wa nchi hiyo na baadhi ya wanavezuela. Bwana [...]

26/02/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mradi wa bidhaa zitokanazo na maziwa zabadili maisha ya Kaya Arusha

Kusikiliza / Kiwanda cha bidhaa za maziwa kilichoko nchini Tanzania

Harakati za kutekeleza malengo ya maendeleo ya Milenia zinazidi kushika kasi kila uchao kuhakikisha ukomo wake unapofikia mwaka 2015, malengo yote manane yanakuwa yametekelezwa. Nchini Tanzania, wadau mbali mbali ikiwemo Uholanzi imeshika kasi kupigia chepuo jitihada hizo, mathalani kutokomeza umaskini kwa kuinua kipato, kuwezesha wanawake kiuchumi na hata elimu kwa watoto kupitia mradi wa kutengeneza [...]

26/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

OPCW yakaribisha usafirishaji wa gesi kama hatua kutokomeza silaha za kemikali

Kusikiliza / Sigrid Kaag, Mratibu maalum wa jopo la pamoja la UM na OPCW

Mratibu maalum wa jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na OPCW kuhusu Syria Sigrid Kaag leo amekaribisha usafirishaji wa gesi ya haradali kutoka Syria kama hatua muhimu katika kutokomeza silaha za kemikali nchini humo . Katika taarifa yake Bi. Kaag amesema jopo hilo lina matumaini ya kusafirisha bidhaa za kemikali zilizoko nchini Syria kwa [...]

26/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utapiamlo kuathiri watoto walioko vitani CAR

Kusikiliza / Utapiamlo CAR

  Vita vinavyoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR zimedhihirisha athari za moja kwa moja ambako ukiachilia mbali athari za kiuchumi, athari za kijamii kama magonjwa hususani kwa watoto zimeanza kujitokeza. Ripoti ya Grace Kaneiya inaangazia namna vita hivyo vya kidini vilivyoigawa jamii hiyo lakinji kubwa zaidi watoto wako katika mazingira hatarishi. Ungana naye.

26/02/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa Ufilipino, juhudi zaidi zahitajika: OCHA

Kusikiliza / Valerie Amos

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu OCHA Valerie Amos ambaye yuko katika zaira nchini Ufilipino nchi ambayo ilikumbwa na kimbunga Typhoon Haiyan ametembelea Giana na Tacloban maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga hicho na kukiri miezi mitatau baada ya kuitembelea nchi hiyo hatua zimepigwa katika kusaidia jamii zilizoathirika. Akiongea na waandishi wa [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata wakabili mpango wa UNDP kuondoa mabomu ya ardhini Cambodia

Kusikiliza / (UNDP/Chansok Lay)

Shirika la mpango wa maendeleo la UM (UNDP) limeelezea wasiwasi wake juu ya upungufu wa wahisani wa kusaidia mpango wa kuondoa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Cambodia. Nchi hiyo imeathirika kutokana na mabaki ya mabomu hayo baada ya miaka 30 ya vita uliomalizika katika miaka ya tisini. Ingawa utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa karibu [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kiwanda cha maziwa eneo la wafugaji laboresha maisha

Kusikiliza / Schola Robert akiwa sehemu ya kutengeneza jibini kwenye kiwanda kinachozalisha bidhaa zitokanazo na maziwa mkoani Arusha

Mradi wa viwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa hususan kwenye maeneo ya wafugaji nchini Tanzania umekuwa na manufaa katika kuboresha maisha ya jamii na kuwezesha kaya kukidhi mahitaji muhimu ikiwemo lishe bora na hata elimu kwa watoto wao. Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha habari nchini humo kilipata taarifa hizo wakati wa mahojiano [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watibuaji wa amani Yemen sasa kukumbwa na vikwazo: Azimio

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Hatua zijazo kuhusu mchakato wa kisiasa nchini Yemen zimepatiwa chepuo hii baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuhusu nchi hiyo likichukua hatua dhidi ya yeyote atakayekwamisha amani, usalama na utulivu wa nchi hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Suala la Yemen lilikuwa ajenda ya kwanza kwenye kikao [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauaji ya wanachuo Nigeria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa  mamia ya wanafunzi huko Yobe nchini Nigeria. Wanafunzi hao waliokuwa katika chuo cha Buni Yadi kilichoko Kaskazini wa Nigeria waliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Kupitia msemaji wake, Ban ameeleza namna alivyosikitishwa na mauwaji hayo na amesema kuwa anamini wahusika [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria ya kupinga ushoga nchini Uganda ni majanga makubwa- Global Fund

Kusikiliza / Global Fund

Mpango wa kimataifa unaojulikana kama Global Fund umelaumu hatua ya kusainiwa kwa sheria inayowabinya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda na kusema kuwa hatua hiyo inazisha mashaka makubwa. Rais wa Uganda Yoweri Mseveni hapo jana alisaini rasmi sheria hiyo ambayo inatoa kifungu cha hadi miaka 7 kwa mtu atayebainika kushiriki vitendo vya ushoga. [...]

26/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNDP yaanzisha mpango wa kuijenga upya CAR

Kusikiliza / Watu wa CAR

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP,limezindua mpango unaogharimu dola za Marekani milioni 26 kwa ajili ya kuendeleza majukumu ya ujenzi wa amani katika taifa la Jamhuri ya Kati.George Njogopa na taarifa kamili. (Taarifa ya George) Mpango huo wa miaka miwili ulizinduliwa leo mjini Bangui unashabaha ya kujenga jamii yenye maridhiano na kufufua matumaini [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani shambulio dhidi ya raia huko Yemen

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu Navi Pillay amelaani shambulio la leo lililofanywa na vikosi vya kijeshi vya Yemen bila ya uangalifu baada ya kukabiliwa na shambulio kusini mwa nchi hiyo. Inaripotiwa kuwa kwenye tukio hilo jeshi la Yemen lilirusha makombora kwenye mji wa Al Dhale na kuua raia saba huku wanane wakijeruhiwa baada ya [...]

26/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031