Nyumbani » 19/02/2014 Entries posted on “Febuari 19th, 2014”

Tanzania yakaza mwendo kufanikisha malengo ya milenia

Kusikiliza / Balozi Mero alipokutana na Dkt. Chan mjini Geneva, Uswisi

Wakati zikiwa zimesalia siku zisizozidi elfu moja kufikia kikomo cha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015 mwakilishi wa kudumu wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva balozi Modest Jonathan Mero amesema sekta ya afya inahitaji msukumo zaidi katika kutekeleza malengo hayo. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Balozi Mero ambaye hivi [...]

19/02/2014 | Jamii: Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Mafunzo kwa jeshi, Somalia

somalia military training

19/02/2014 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Usalama Sudan Kusini

Usalama_Sudan_Kusini

19/02/2014 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mafunzo kwa jeshi, ishara ya kuimarika kwa nchi: Somalia

Kusikiliza / Wakati wa mafunzo kwa jeshi la Somalia

Wakati taifa la Somalia likiwa linajimarisha katika nyanja mbalimbali ujenzi wa taifa hilo unahusisha sekta ya ulinzi ambapo mkakati wa hivi karibuni zaidi ni mafunzo kwa jeshi hilo mafunzo yanayofanywa chini ya uratibu wa vikosi vya muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM. Ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo

19/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Dujarric awa msemaji mpya wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Stéphane Dujarric

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemteua Stéphane Dujarric kuwa msemaji mpya wa Umoja wa Mataifa akichukua nafasi ya Martin Nesirky ambaye ameamua kuachia nafasi hiyo na kuwa karibu na familia yake hukoVienna, Austria ambako hata hivyo ataendelea na kazi ndani ya Umoja huo. Akitangaza uteuzi huo mbele ya waandishi wa habari hii leo, Bwana [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya afya ni muhimu kuelekea kikomo cha MDGS : Balozi Mero

Kusikiliza / Balozi Mero akiwa na Mkuu wa UM Geneva

Wakati zikiwa zimesalia siku zisizozidi elfu moja kufikia kikomo cha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015 mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, balozi Modest Jonathan Mero amesema sekta ya afya inahitaji msukumo zaidi katika kutekeleza malengo hayo. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Balozi [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa iunge mkono UM katika kuimarisha utawala wa sheria

Kusikiliza / Maafisa wa mahakama nchini DRC wakipatiwa mafunzo kwenye semina zinazoendeshwa na MONUSCO kuimarisha vyombo vya haki nchini humo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa kuanza kwa mjadala kuhusu uendelezaji na uimarishaji wa utawala wa kisheria na amani ya usalama duniani akitaka jamii ya kimataifa kusaidia juhudi hizo. Taarifa zaidi na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Mjadala huo unazingatia ripoti ya Katibu [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay awaonya viongozi CAR

Kusikiliza / Wananachi wa CAR

Huku hali ya mashafuko ikiendelea kuangamiza maisha ya raia wasio na hatia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay  amewakumbusha viongozi walioko kwenye vyombo vya mamlaka kuwa wanawajibu wa kisheria na akawaambia kwamba iko siku watawajibika kutokana na uhalifu wa kibinadamu unaoendelea. Taarifa zaidi [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO  yafafanua kuhusu kuenea kwa virusi vya A(H7N9

Kusikiliza / FAO yafuta madai ya awali ya maambukizi ya homa ya ndege kutoka kwa ndege hadi binadamu

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO limesema kuwa hakuna ushahidi wowote unaonyesha kwamba binadamu aliyeathiriwa na virusi vya homa ya mafua ya ndege  A(H7N9), alipata maambukizi kutoka kwa wanayama lakini kuna kiwango kidogo cha virusi kinaweza kuambukizwa kwa wanyama ikiwemo jamii ya ndege. Taarifa hiyo ya FAO imekumbusha juu ya tukio la mtu mmoja kuathiriwa [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitikia kuzorota kwa hali ya haki za binadamu Korea Kaskazini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado anaendelea kusalia katika hali ya wasiwasi mkubwa kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Korea ya Kaskazini. Ameeleza hali hiyo kufuatia ripoti iliyotolewa na kamishna maalumu iliyokwenda nchini humo kuchunguza juu ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Ban [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka kuepukwa matumizi ya nguvu zaidi kwenye mzozo wa Ukraini

Kusikiliza / Navi Pillay

Huku hali ya ghasia ikiendelea kuchacha nchini Ukraine, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amezitaka pande zilizojitumbukiza katika machafuko kujiepusha na matumizi makubwa ya nguvu. Kauli hiyo imekuja katika wakati ambapo ripoti zikisema kuwa zaidi ya jumla ya watu 22 wamepoteza maisha wakati kulipozuka mapigano baina ya waandamanaji na [...]

19/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Plumbly alaani mashambulio yaliyotokea huko Lebanon

Kusikiliza / Derek Plumbly

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amelaani mashambulio mawili yaliyotokea leo kwenye kitongoji cha Bir Hassan in kilicho kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababsiha vifo na majeruhi kadhaa. Katika taarifa yake, Bwana Plumbly ametuma rambirambi kwa familia za marehemu na kuwatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa. Licha ya shambulio [...]

19/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031