Nyumbani » 18/02/2014 Entries posted on “Febuari 18th, 2014”

Mbwa watumika kumiarisha ulinzi kwa raia Sudani Kusini

Kusikiliza / Mbwa wakiwa kazini

Wakati hali ya machafuko ikiendelea nchini Sudani Kusini ulinzi hususani kwa raia ni changamoto kubwa kwa sasa. Umoja wa Mataifa ambao licha ya juhudi ambazo unachukua kuhakikisha machafuko yanakomeshwa unachukua hatua stahiki za ulinzi na sasa wanyama mbwa wanatuika wka ajili ya ulinzi nchini humo.   Ungana na Joseph Msami katika ripoti inayofafanua zaidi   [...]

18/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka hatua ya dharura ichukuliwe kufuatia ripoti kuhusu DPRK

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameikaribisha ripoti ilotolewa Jumatatu na tume huru kuhusu haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, na kusema kuwa matokeo yake yanatakiwa kuchukuliwa kama jambo la dharura. Bi Pillay ameongeza kuwa matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa uhalifu dhidi [...]

18/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Njaa kali yaikumba Somalia, misaada ya dharura yahitajia: UM

Kusikiliza / John Ging akihutubia waaandishi wa habari (Picha ya makataba)

Hali mbaya ya kiutu inayosababishwa na njaa nchini Somalia ni lazima itatuliwe kwa kuchangisha fedha zaidi ili kukomboa kuwa watu takribani milioni mbili ambao hawana uhakika wa chakula. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York mkuu wa opereseheni za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Bwana John [...]

18/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viongozi waandamizi wa UM ziarani CAR, IOM yatoa matokeo ya tathmini kwa wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / Wananachi wa CAR

Mratibu Mkuu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Bi. Valerie Amos ameanza ziara ya mbili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati akiwa ameambana na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe na Kamishna wa masuala ya siasa ndani ya Muungano wa AFrika Dkt. Aicha L. Abdullahi. Habari zinasema wakiwa [...]

18/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza kuu lajadili maji, usafi na nishati endelevu

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya kikao leo kujadili kuhusu maji, usafi na nishati endelevu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Joshua Mmali amekuwa akifuatilia kikao cha leo TAARIFA YA JOSHUA MMALI Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe ameliambia baraza hilo kuwa matatizo ya maji, usafi, nishati endelevu ndiyo changamoto kuu [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahaha kukomboa watoto katika machafuko Iraq

Kusikiliza / Nembo ya UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na lile la wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepeleka misada ya vifaa vya kuokoa maisha ya watoto na wanawake waliokumbwa na ghasia katika jimbo la Anbar nchini Iraq. Hii ni awamu ya tatu ya msaada huu ambapo mwakilishi wa UNICEF [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mauaji vijijini Nigeria

Kusikiliza / human rights council

Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, imelaani vikali mashambulizi yalotekelezwa mnamo Jumapili na watu wenye silaha dhidi ya vijiji 8 katika majimbo ya Adamwa na Borno, nchiniNigeria, na kuwaua watu zaidi ya 150.  Ripoti zinasema watu wapatao 65 waliuawa katika vijiji 7 kwenye jimbo la Adamwa, huku wengine 90 wakiuawa katika kijiji [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafua ya ndege yasababisha kifo kimoja China, huko Malaysia nako kisa kimoja charipotiwa

Kusikiliza / Homa ya mafua ya ndege inayodaiwa kusababishwa na kirusi A(H7N9) kutoka kwa ndege

Nchini China homa ya mafua ya ndege isababishwayo na kirusi aina ya A(H7N9) imeendelea kuwa tishio ambapo imesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine Tisa wamethibitishwa kuambukizwa. Shirika la Afya duniani, WHO limesema limepata uthibitisho kutoka tume ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini China ambayo imesema kuwa wagonjwa hao kwenye majimbo ya [...]

18/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapata hofu juu ya mustakbali wa wasaka hifadhi huko Manus, Papua New Guinea

Kusikiliza / Papua New Guinea

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema lina hofu kubwa juu ya kile kinachoendelea kwenye kisiwa cha Manus huko Papua New Guinea, eneo ambako wamehamishiwa baadhi ya watu waliokuwa wanasaka hifadhi nchini Australia. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (Taarifa ya Alice) UNHCR inasema hofu hiyo inatokana na taarifa ya kwamba msaka hifadhi [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sintofahamu yakumba raia wa Uganda juu ya Muswada kuhusu mapenzi ya jinsia moja

Kusikiliza / Ramana ya Uganda

Nchini Uganda wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja baada ya baadhi ya nchi za magharibi kuendelea kutishia kuondoa misaada pale sheria hiyo itakapotiwa saini na Rais Yoweri Museveni. Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inawapatia kifungo cha maisha jela wapezi wa jinsia moja. Awali alikataa sheria hiyo akisema adhabu [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yataka Uganda kutupilia mbali sheria dhidi ya mashoga

Kusikiliza / Michel Sidibé

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS nalo limepaza sauti dhidi ya muswada wa sheria wa kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda likisema ukiwa sheria utasababisha ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kinyume na haki za binadamu. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé amesema Uganda ilikuwa nchi ya [...]

18/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930