Nyumbani » 15/02/2014 Entries posted on “Febuari 15th, 2014”

Ban atoa heko kwa Lebanon kwa kuunda serikali mpya

Kusikiliza / Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha tangazo la kuundwa kwa serikali mpya nchini Lebanon leo, na kumpa heko Waziri Mkuu Tamam Salam kwa hatua hiyo muhimu. Taarifa ilotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amewahimiza viongozi wa kisiasa wa Lebanon kuendeleza mazungumzo ya kujenga yalochangia kuundwa kwa serikali hiyo [...]

15/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa washindwa tena kugawa misaada ya dharura kwenye kambi ya Yarmouk, Syria

Kusikiliza / kambi ya yarmouk mjini Damascus

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limesema kuwa hii leo limeshindwa tena kugawa misaada ya chakula na vifaa vingine vya kibinadamu katika kambi ya Yarmouk, iliyoko Damascus. Msemaji wa UNRWA, Chris Gunness, amesema kuwa UNRWA haijaweza kugawa chakula katika kambi hiyo kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa, [...]

15/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa masuala ya kisiasa wa UM ahitimisha ziara nchini Afghanistan

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman amekamilisha ziara ya siku mbili nchini Afghanistan hii leo, ambayo imekuwa ziara yake ya kwanza nchini humo tangu alipochukuwa wadhfa wa kusimamia masuala ya kisiasa mnamo Julai 2, 2012. Katika ziara hiyo, Bwana Feltman amejikita katika kupata uelewa wa majukumu ya ujumbe wa Umoja wa [...]

15/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya Syria yamalizika bila maendeleo yoyote, Brahmi aomba radhi wasyria

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kuhusu Syria iliyokuwa inafanyika huko Geneva, Uswisi imemalizika bila maendeleo yoyote huku msuluhishi mkuu Lakhdar Brahimi akiomba radhi wananchi wa Syria kwa kitendo hicho. Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa wiki mbili yalikutanisha pande zinazohasimiana nchini Syria ikiwemo serikali na upinzani ambapo Brahimi amesema pande hizo zimeshindwa kukubaliana juu ya [...]

15/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930