Nyumbani » 07/02/2014 Entries posted on “Febuari 7th, 2014”

Mapigano Homs yasitishwa kwa siku tatu, huduma za usaidizi zafikishwa: UM

Kusikiliza / Watoto wa Syria huko Homs.

Watu 83 wamehamishwa kutoka mji wa Homs huko Syria wakati wa siku tatu za kusitisha mapigano zilizokubaliwa kati ya pande husika kwenye mzozo huo ili huduma za usaidizi wa kibinadamu ziweze kuingizwa. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq akizungumza mjini New York amethibitisha ripoti za vyombo vya habari ya kwamba mapigano yalisitishwa Homs na [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukeketaji mkoani Mara, Tanzania wadaiwa kufanywa na baadhi ya wauguzi.

Kusikiliza / Watoto kwenye kampeni dhidi ya ukeketaji watoto wa kike na wanawake

Tarehe Sita Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketeji wa watoto wa kike na wanawake. Takwimu zaonyesha kuwa kila mwaka watoto Milioni Tatu wako hatarini kukumbwa na mila hiyo potofu barani Afrika na huko Mashariki ya Kati inakotendwa. Shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA linasema cha kutia shaka zaidi kitendo hicho [...]

07/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wavuvi mkoani Tanga, Tanzania waeleza wanavyonufaika na radio

Kusikiliza / Shughuli ya uvuvi mkoani Tanga

Huko mkoani Tanga Tanzania, moja ya mikoa iliyoko pembezoni mwa bahari ya Hindi nchini humo, uvuvi ni moja ya shughuli kubwa . Je wavuvi wanazungumziaje mahusiano yao na radio? Inawanufaisha vipi? Ungana na Richard Katuma wa radio washirika Pangani Fm kutoka mkoani humo katika makala ifuatayo.

07/02/2014 | Jamii: Makala za wiki, Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni sasa kupitia michezo

Kusikiliza / Wanariadha waliodhaminiwa na UNFPA Tanzania na kushiriki mbio ndefu za Kilimanjaro (Picha-UNFPA)

Katika hatua za kupambana na mimba na ndoa za utotoni shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania limeamua kutumia mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii kupinga vitendo hivyo vinavyoelezwa kuwa na atahari za kiafya na kijamii. Mtaalamu wa masuala ya jinsia wa UNFPA [...]

07/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yasafirisha wahamiaji wa Rwanda waliofurushwa Tanzania

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa msaada wa dharura kwa zaidi ya raia wa Rwanda 15,000 waliorudishwa kutoka Tanzania kwa kipindi cha miezi sita iliyopita. Mkuu wa IOM nchini Rwanda Catherine Northing amesema inakadiriwa kuwa wanyarwanda ambao hawana vibali vya kuishi wamefurushwa licha ya kwamba idadi ya wahamiaji hao wanaowasili mipakani ni ndogo kwa [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wa dunia ni muhimu kudhibiti utoroshaji wa fedha kutoka Afrika

Kusikiliza / Thabo Mbeki

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa katika kuhakikisha suala la utoroshaji wa fedha kutoka Afrika linatokomezwa. Mbeki ambaye ni mwenyekiti mwenza wa jopo la Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika na Muungano wa Afrika amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani. Amesema [...]

07/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunaanza uchunguzi wa awali huko Jamhuri ya Afrika ya Kati: ICC

Kusikiliza / Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda

Mwendesha mashtaka mkuu kwenye Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai huko The Hague Uholanzi, Fatou Bensouda ametangaza kufungua upya kwa uchunguzi wa kile kuendelea huko Jamhuri ya Afrika kati, CAR kutokana na tuhuma zinazoibuka kila uchao juu ya madhila ya mateso yanayokumba raia. Katika taarifa yake hii leo Bi. Bensouda ametaja tuhuma hizo kuwa [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vifo vitokanavyo na surua vimepungua kwa kiwango kikubwa zaidi: WHO

Kusikiliza / surua, Burundi

      Idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa surua kila mwaka imeshuka kwa asilimia 77 kutoka mwaka 2002 hadi mwaka 2012, na hivyo kuzuia zaidi ya vifo milioni 13, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO. WHO imetangaza hayo wakati wa uzinduzi wa ripoti yake ya makadirio ya vifo vitokanavyo na surua. Ugonjwa wa [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na viongozi kadhaa wakati michezo ya Olimpiki ikianza Sochi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akipatiwa maelezo alipotembelea kijiji cha Olimpiki huko Sochi, Urusi

Mashindano ya michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi yanang'oa nanga huko Sochi Urusi jioni ya leo, yakihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon. Wakati wa kuanza michezo hiyo, ujumbe wa video wa Katibu Mkuu utaonyeshwa kwenye sherehe ya ufunguzi. Tayari leo, Bwana Ban amekutana na viongozi kadhaa wanaohudhuria sherehe hiyo, wakiwemo [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa kuchunguza athari za matangazo ya biashara kwa haki za utamaduni

Kusikiliza / Farida Shaheed

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za utamaduni, Farida Shaheed, amezindua utafiti mpya katika athari za matangazo ya biashara kwenye haki za tamaduni za watu. Utafiti huo utazingatia hasa athari za matangazo hayo kwenye utofauti wa tamaduni na haki za binadamu. Ataangazia pia athari za ufadhili wa kibiashara kwenye haki miliki za usomi [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Miezi mitatu baada ya tetemeko la ardhi Ufilipino hali ya kibinadamu bado si shwari: OCHA

Kusikiliza / Tetemeko la ardhi huko Bohol liliharibu makazi mengi.

Miezi mitatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga eneo la Bohol nchini Ufilipino, hali ya kibinadamu bado si nzuri na mahitaji bado ni makubwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi wa kibinadamu OCHA. Mathalani wengi wa watu zaidi ya Laki Tatu na Nusu ambao nyumba zao ziliharibiwa au kuteketezwa kabisa bado wanaishi [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia CAR zasababisha maelfu kukimbilia Cameroon

Kusikiliza / Hatma ya watoto hawa wakimbizi kutoka CAR iko mashakani kutokana na mapigano nchini mwao.

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamekimbilia Cameroon katika siku chache zilizopita kutokana na mapigano kati ya vikundi vya waasi vinavyopingana na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kama anavyoripoti Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Katika siku Kumi zilizopita watu 9,000 wamewasili Kentzou, [...]

07/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031