Nyumbani » 06/02/2014 Entries posted on “Febuari 6th, 2014”

Mapambano dhidi ya ukeketaji Tanzania, safari ni ndefu lakini kuna matumaini.

Kusikiliza / Wasichana kama hawa wasikeketwe!

Dunia ikiwa inaadhimisha siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na wasichana inaelezwa kuwa mila na desturi ni kikwazo kikubwa katika harakati za kutokomeza vitendo hivyo. Katika mahojiano na Joseph Msami wa  idhaa hii Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA nchini Tanzania, Christine Kwayu amesema licha [...]

06/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kusuasua kwa ratiba ya kuharibu mpango wa kemikali Syria kwatia wasiwasi:

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama la UM kwa mwezi Februari Balozi Raimonda Murmokaitė kutoka Lithuania

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wamesikiliza ripoti ya maendeleo ya kazi ya kuharibu mpango wa silaha za kemikali wa Syria ambapo wameonyesha wasiwasi wake juu ya kusuasua kwa utekelezaji wa ratiba husika. Ripoti hiyo iliwasilishwa na Mratibu wa jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wakaribisha kuondolewa vikwazo kwa raia walionaswa Syria

Kusikiliza / Valirie Amos

Umoja wa Mataifa umekaribisha taarifa kwamba pande zinazohasimiana nchini Syria zimeruhusu raia kutoka na kuruhusu misaada kuwasili katika mji wa kale uitwao Homs. Mratibu wa ugawaji wa misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos amekaribisha hatua hiyo kwa kusema atafuatilia maendeleo ya hatua hiyo ambayo itaruhusu raia kurejea makwao na msaada wa kuokoa [...]

06/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Radio ni mkombozi kwa wanawake DRC

Kusikiliza / Studio za radio ya Umoja wa Mataifa

  Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , DRC radio ni chombo chenye umuhimu mkubwa hususani kwa wanawake, ambao wanasema wanapata elimu, kuhusu masuala ya uzazi na mengineyo ya kijamii. Ungana na Langi Asumani wa radio washirika Umoja nchini humo aliyefanya mahojiano na Sango Batenji, mratibu wa shirika la FFD Baraka akiangazia umuhimu wa radio [...]

06/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Iraq, likiwemo lile dhidi ya Wizaza ya Mambo ya Nje hapo jana. Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulizi hayo na kuwatakia walojeruhiwa nafuu haraka. [...]

06/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ufugaji wa samaki kuwa mkombozi ifikapo mwaka 2030

Kusikiliza / Ufugaji wa samaki

Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa imeweka bayaan kuwa ufugaji wa samaki utachangia karibu theluthi mbili ya kitoweo cha samaki duniani ifikapo mwaka 2030. Benki ya dunia, Shirika la chakula na kilimo duniani FAO na lile la kimataifa la utafiti wa sera za chakula yamesema hali hiyo inatokana na kupungua kwa samaki wanaovuliwa [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utapia mlo huenda ukakatili maisha ya watoto 50,000 Mali:UM

Kusikiliza / Mtoto mwenye utapiamlo

Mashirika ya misaada nchiniMaliyameelezea hofu yake juu ya kiwango kikubwa cha utapiamlo nchiniMalina kuonya kuwa watoto wapatao 50,000 wanaweza kufariki dunia mwaka huu. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi (TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI) Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Mali David Gressely amesema anasema ufadhili wa haraka unahitajika ili kupeleka bidhaa za lishe katika maeneo [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asifu uwezo wa michezo kuleta watu pamoja

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Rais wa IOC Thomas Bach

Huku ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuanza mashindano ya Olimpiki ya Msimu wa baridi huko Sochi, Urusi, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema michezo ina uwezo wa kuwaleta watu pamoja, kwani inavuka mipaka yote, huku akitoa wito wa amani ya Olimpiki kwa wote wanaozozana. Joshua Mmali na taarifa kamili Taarifa ya Joshua Bwana Ban amesema [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tulinde tamaduni nzuri zile potofu tuachane nazo: Ban

Kusikiliza / Bango la kampeni dhidi ya Ukeketaji wanawake na watoto wa kike

Tunapaswa kulinda mazuri yote kwenye tamaduni zetu na kuachana na zile ambazo zinatuathiri, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye ujumbe wake wa siku ya kutokomeza ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike hii leo. Amesema hakuna sababu yote iwe ya kiafya, kimaendeleo au kidini ya kuendeleza mila hiyo potofu na kwa [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kunyima watu chakula, maji, malazi na huduma za afya vyatumika kama mbinu ya vita Syria:

Kusikiliza / Watoto wakimbizi nchini Syria wakabiliwa na uhaba wa mahitaji ya msingi

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula, afya, nyuma, maji , usafi na mauaji na utesaji Alhamisi wamezitaka pande zote zinazohasimiana katika vita vya Syria kukoma mara moja kutumia madhila ya raia kama mbinu ya vita. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Wataalamu hao wamesema wakati taarifa [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA na serikali ya DRC leo kuzindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu

Kusikiliza / Baada ya amani kurejea Mashariki mwa DRC, wanawake wana matarajio makubwa ya ustawi

Shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi wa kibinadamu, OCHA kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo Alhamisi wanazindua mpango wa usaidizi wa kibinadamu nchini humo. Mwandishi wa Radio Okapi Jean-Pierre Elali Ikoko amemkariri Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko DRC kwa masuala ya usaizidi wa binadamu [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi tatu za Afrika zapongezwa kwa kuchukua hatua dhidi ya Ukeketeaji wanawake

Kusikiliza / Kampeni ya kutokomeza ukeketaji watoto wa kike na wanawake

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa watu, UNFPA limetoa heko kwa Uganda, Kenya na Guinea-Bissau kwa kutunga sheria zinazoharamisha ukeketaji. Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde Osotimehin katika ujumbe wake wa siku ya leo amesema hayo ni mafanikio wakati [...]

06/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031