Nyumbani » 05/02/2014 Entries posted on “Febuari 5th, 2014”

Shambulio dhidi ya wizara ya mambo ya nje ya Iraq lalaaniwa na UM:

Farhan Haq

Shambulio dhidi ya ofisi za wizara ya mambo ya nje yaIraqambalo limekatili maisha ya watu na kujeruhi wengine limelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa. Imearifiwa kwamba mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa kwenye magari yameripuka nje ya wizara ya mambo ya nje mjiniBaghdadsiku ya Jumatano. Machafuko ya kidini yameshika kasi mwaka jana nchiniIraq. Kwa mujibu wa msemaji [...]

05/02/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yaonya makundi ya silaha dhidi ya kuwashambulia wahudumu wake

Walinda amani wapiga doria DRC

Makundi yenye silaha katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, yameonywa kuhusu kufanya mashambulizi dhidi ya  wahudumu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO. Onyo hilo limetolewa na Jemedari Abdallah Wafy, ambaye ni Naibu Mwakilishi maalum wa katibu mkuu na Mkuu wa MONUSCO, ambaye pia ndiye msimamizi wa idara [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Radio imekuwa chombo cha thamani kwa wanawake wakulima huko Sengerema, Tanzania

kilimo

  Katika kuelekea siku ya Radio duniani tarehe 13 mwezi huu, tathmini mbali mbali zimeendelea kufanyika kubaini uwezeshaji wa jinsia kupitia Radio. Mathalani, makundi ya wanawake yamenufaika vipi kupitia Radio? Wawe ni wasikilizaji au ni watendaji.. Mwenzetu Pauline Mpiwa wa Radio Washirika Sengerema FM iliyoko Mwanza nchini Tanzania aliamua kuangazia wanawake wakulima kuona wao Radio [...]

05/02/2014 | Jamii: Makala za wiki, Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Hukumu dhidi ya Katanga yasogezwa mbele mwezi mmoja

Germain Katanga

Mahakama ya Kimataifa ya  makosa ya jinai, ICC  huko The Hague, Uholanzi imesogeza mbele kwa mwezi mmoja zaidi tarehe ya kusomwa hukumu dhidi ya Germain Katanga kutokana na mmoja wa majaji kupata udhuru wa kiafya.   Taarifa ya ICC imesema hukumu hiyo ilikuwa isomwe Ijumaa hii tarehe Saba lakini sasa itasomwa tarehe Saba mwezi ujao. [...]

05/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini imetakiwa kukabiliana na chanzo cha machafuko:

Bwana Ladsous akisalimiana na baadhi ya wananchi alipotembelea Juba, Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imetakiwa na Umoja wa Mataifa kukabiliana na mizizi ambayo ni chanzo cha vita vinavyoendelea ili kuleta amani katika taifa hilo changa. Sudan Kusini inashuhudia machafuko ya ndani ynayoendelea baada ya majeshi yanayomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais kubeba silaha na kuanza kupambana na serikali mwishoni mwa Desemba mwaka jana. Akizungumza [...]

05/02/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya huduma ya afya imeimarika Afrika Magharibi:UNFPA

Mama akichunguzwa afya yake kwenye moja ya vituo vya afya ya mama na mtoto nchini Sierra Leone. (Picha-UNFPA)

Matokeo ya awali yaliyotolewa wiki hii kuhusiana hali za kaya na afya nchini Sierra Leone yanaonyesha kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa kwa kuboresha mifumo ya utoaji huduma za kiafya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ripoti hiyo ya matokeo inasema kuwa kwa kulinganisha na tafiti zilizopita taifa hilo limefanikiwa kuboresha huduma zake hasa katika [...]

05/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM umelaani mauaji ya mfanyakazi wake DR Congo:

Martin Kobler. Picha ya UN

Mauaji ya mfanyakazi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO yamelaaniwa vikali na na maafisa wawakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Mfanyakazi huyo alipigwa risasi na kuuawa mjini Beni huko Kivu ya Kaskazini leo Jumatano asubuhi wakati akielekea kazini. Mji wa Beni ambao uko [...]

05/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2013 ni miongoni mwa 10 iliyokuwa na joto kali zaidi:WMO

Kimbunga Haiyan mojawapo ya mambo yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa

Mwaka 2013 ulikuwa miongoni mwa miaka iliyokuwa na joto kali saana tangu kuanza kuwekwa kumbukumbu ya wiwango vya joto mnamo mwaka 1850, limesema shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO. Taarifa ya Flora Nducha Inafafanua (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Kwa mujibu wa shirika hilo mwaka jana umefungana na mwaka 2007 kama miaka [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati kuhusu haki za mtoto yaitaka Holy See kutoficha uhalifu dhidi ya watoto

Baraza la Haki za binadamu ambalo kamati ya haki za watoto ni mojawapo ya kamati zake.

Kamati ya kimataifa kuhusu haki za watoto imeelezea kusikitishwa na hatua za kuwahamisha mapadri wanaotenda ukatili wa kingono dhidi ya watoto kutoka parokia moja hadi nyingine au kutoka nchi moja hadi nyingine ili kujaribu kuvificha vitendo hivyo ambavyo vimeripotiwa na tume kadhaa za kitaifa za uchunguzi. Hayo yameibuka huko Geneva, Uswisi wakati kamati hiyo ikihitimisha tathmini [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yaonya kuhusu tishio la njaa Sudan Kusin

Wasudan Kusini waliolazimika kusaka makazi ofisi za UM ili kukimbia mapigano

Shirika la chakula na kilimo duniani,  FAO limeonya juu ya uwezekano wa kujitokeza kwa hali mbaya ya ukosefu wa chakula huko Sudan Kusini ambako kiasi cha watu milioni 3.7 wako katika hali ngumu wakihitaji misaada mbalimbali ikiwemo chakula. Taarifa kamili na George Njogopa. (George Njogopa) FAO imetoa mwito ikihitaji kiasi cha dola za Marekani milioni [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hispania yahimizwa kuziamini vyombo vyake vya maamuzi

Pablo de Greiff

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa Pablo de Greiff ameiambia Hispania kwamba haipaswi kuwa na wasiwasi juu ya vyombo vyake vya utoaji maamuzi na kwamba haina haja ya kuhairisha mchakato wake unaolenga kuwatendea haki waathirika wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilivyofanywa na dikteta Franco wakati kulipuzuka machafuko ya kiraia. Joseph Msami na maelezo [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto Syria wanakabiliwa na madhila yasiyoelezeka:UM

Watoto wa Syria wakiwa na wazazi na walezi wao (Picha-UNHCR)

Watoto nchini Syria wamekuwa wakikabiliwa na madhila yasiyoelezeka kwa karibu miaka mitatu sasa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imesema ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi vita vinavyoathiri vijana. Ripoti hiyo inaishutumu serikali ya Syria na washirika wake ambao ni wanamgambo kwa kuhusuka na mauaji yasiyohesabika pamoja na ukatili na utesaji wa [...]

05/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031