Nyumbani » 04/02/2014 Entries posted on “Febuari 4th, 2014”

Takribani miaka 20 baada ya mkutano wa Beijing, wanawake bado wanakumbwa na madhila: Ban

Kusikiliza / Mkutano wa Beijing wa wanawake(picha ya maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mwaka 2015 ni mwaka muhimu sana ambao pamoja na kuwa ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia, pia ni miaka 20 tangu mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing ulioweka mwelekeo wa hatua za usawa wa kijinsia. Bwana Ban amesema hayo baada ya tukio maalum la [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo 490 vimesababishwa na mapigano ya kikabila nchini Kenya 2013:OCHA

Kusikiliza / Nembo ya OCHA

Takriban watu 490 wamepoteza maishayaokatika machafuko ya kikabila Kaskazini mwa Kenya mwaka 2013 imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA. Shirika hilo linasema zaidi ya watu wengine 1,200 walijeruhiwa na wengine zaidi ya 47,000 kulazimika kuzikimbia nyumba zao. Limeongeza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la mapigani kwa mwezi wa Desemba. [...]

04/02/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lahitimisha ziara yake nchini Mali

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la usalama wakilakiwa nchini Mali

Uwanja wa ndege wa Bamako nchini Mali, ndege ya Umoja wa Mataifa iliyobeba wajumbe wa Baraza la Usalama ikiwasili tayari kwa ziara maalum nchini humo. ….. Mwenyeji hapa ni Bert Koenders, mwakilishi maalum kwa Katibu Mkuu wa UM nchini Mali na mjumbe mmoja baada ya mwingine anatambulishwa kwa viongozi wa serikali na wale wa Umoja [...]

04/02/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania,Australia kuongoza mjadala siku ya radio duniani.

Kusikiliza / Nembo

Tukiwa tunaelekea siku ya radio duniani tarehe 13 mwezi huu, mratibu wa siku hiyo katika radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amesema mjadala maalum utakaoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO utafanyika katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York huku pia akisema Tanzania na Australia [...]

04/02/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Barizi yarejea kwenye Ufukwe wa Lido Somalia

Kusikiliza / Ufukwe wa Lido nchini Somalia

Nchini Somalia kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kiliendesha vitendo vya vitisho na kubadili mfumo wa maisha ya watu. Mathalani watu waliopenda kubarizi kwenye maeneo ya fukwe kwenye mji mkuu Mogadishu walihofia mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na kundi hilo eneo hilo. Hata hivyo juhudi za Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika zimeleta nuru kwenye maeneo [...]

04/02/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtu mwingine afariki Saudia kutokana na kuambukizwa homa ya Corona

Kusikiliza / Madakatari waangalia picha za x-ray

    Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa mnamo Januari 28, Wizara ya Afya nchini Saudi Arabia ilitangaza kuwa mtu mmoja zaidi amethibitishwa kuambukizwa homa ya kirusi cha corona (MERS-CoV) kufuatia vipimo vya maabara. Mtu huyo ni mwanamume mwenye umri wa miaka 60 kutoka Riyadh, ambaye alianza kuumwa mnamo Januari 19, akiwa na dalili [...]

04/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kila anayeumwa ana haki ya kupata dawa za kupunguza maumivu zilizoidhinishwa: INCB

Kusikiliza / Dawa

Rais wa Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Raymond Yans, amesisitiza umuhimu wa mikataba ya kimataifa ya udhibiti wa madawa hayo katika kuhakikisha kuwa dawa zilizoidhinishwa zipo na zinatumiwa vizuri katika kutuliza maumivu na kuwaondolea wagonjwa machungu. Akizungumza kwenye kikao cha 109 cha bodi hiyo, Bwana Yans amesema watu wote wana haki za [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saratani bado ni changamoto kubaini mapema ndio tiba: WHO

Kusikiliza / Leo ni siku ya saratani duniani

Leo ni siku ya saratani duniani ambapo Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa ugonjwa huo kwa sasa ni chanzo kikuu cha vifo ukiwa umesababisha vifo vya watu Milioni Nane Nukta Mbili mwaka 2012. Saratani zinazoongoza ni ile ya mapafu, tumbo, ini, utumbo mpana na ile ya titi. Ujumbe wa mwaka huu ni vunja ukimya [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuzorota kwa usalama Anbar kwa tishia uingizaji misaada:IOM

Kusikiliza / Kuzorota kwa usalama kunakwamisha shughuli, IOM

Wakati hali ya usalama inaendelea kuzorota Anbar nchini Iraq, misaada inayoingizwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwenye jamii zilizoathirika na machafuko Anbar, Fallujah na Ramadi iko katika hatihati. IOM inasema hali ya usalama katika maeneo hayo haitabirika nay a wasiwasi, huku wenyeji wakisema mapigano yanayoendelea na uvurumishaji wa maroketi hauchagui na umeshasababisha vifo [...]

04/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto zaidi ya 20,000 wataanza masomo CAR:UNICEF

Kusikiliza / Watoto wa jamii ya wafugaji waliopata makazi waenda shule nchini CAR

Watoto zaidi ya 20,000 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wataanza masomo katika madarasa ya muda baada ya machafuko kuwalazimu kuzikimbia nyumba zao na shule zao kufungwa. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakati shule zote katika mji mkuu Bangui zimefungwa tangu mapema Desemba mwaka 2013, shirika hilo na [...]

04/02/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP kuingiza chakula kwa njia ya ndege CAR kufuatia usalama mdogo barabarani:

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula msaada wa WFP nchini CAR

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP litaanza kusafirisha msaada wa chakula kuingia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa njia ya ndege kwa sababu usafiri wa barabara hauaminiki kutokana na usalama mdogo. Flora Nducha na maelezo zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Mpango ni kusafirisha tani 2000 za chakula kingi kikiwa ni mchele kuelekea [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii zaidi zaendelea kuchana na mila potofu ya ukeketaji:UM

Kusikiliza / Watoto hawa wa kike wanapaswa kuepushwa dhidi ya mila potofu ya ukeketaji. (Picha-UNFPA)

Tarehe Sita Februari ndio siku husika ambapo mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la idadi ya watu UNFPA na lile la watoto, UNICEF yamesema harakati hizo zimezaa matunda lakini bado mila hiyo inatekelezwa na hivyo yanatekeleza programu ya kuona jamii zaidi zinaachana nayo. Yamesema kampeni inayohusisha wadau wote ni muhimu kwani baadhi ya [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania na Australia kushiriki mjadala kuhusu siku ya Radio duniani kwenye UM

Kusikiliza / Siku ya Radio duniani

Mratibu wa siku ya radio duniani katika radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amesema katika kuadhimisha siku hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na Tanzania na Australia litaendesha mjadala kuhusu namna radio inavyowezesha jinsia hususani wanawake na wasichana. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Bi Nducha [...]

04/02/2014 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Radio Duniani, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031