Zaidi ya dola Bilioni 2.4 zaahidiwa ili kuikwamua Syria

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na viongozi waandamizi wa UM na Kiongozi Mkuu wa Kuwait kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Kuwait

Mkutano wa pili wa kimataifa wa usaidizi wa kibinadamu kwa Syria umemalizika hukoKuwait ambapo zaidi ya dola Bilioni 2.4 zimechangishwa ikiwa ni ahadi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo amesema kiasi kamili cha fedha kitatangazwa baadaye lakini ahadi hiyo ni ishara dhahiri kuwa wahanga wa mzozo wa Syria hawajasahaulika na ndio maana mashirika na hata nchi zimejitoa kwa hali na mali kusaidia wananchi hao.

Bwana Ban amesema Umoja wa Mataifa utahakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo ili kuwapatia mamilioni ya wahanga wa mzozo wa Syria huduma muhimu kama vile maji, chakula, malazi, matibabu ya dharura na huduma nyingine muhimu.

Katibu Mkuu amesema jumuiya ya kimataifa imejitoa kwa moyo kwenye masuala ya kiutu na sasa kilichobakia ni kuleta pamoja pande zinazozozana Syria ili mkutano wa wiki ijayo huko Uswisi uweze kuzaa matunda.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031