WHO na wadau wazindua kampeni dhidi ya Surua, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua

Baada ya taasisi moja nchini Jamhuri ya Afrika  ya Kati, CAR kuthibitisha uwepo wa wagonjwa wa surua kwenye kambi mbili za wakimbizi wa ndani nchini humo, mashirika ya umoja wa Mataifa na wadau wamezindua kampeni ya dharura ya kudhibiti ugonjwa huo.

Mashirika hayo ni pamoja na lile la afya, WHO, watoto UNICEF na lile la madaktari wasio na mipaka, MSF ambapo kampeni hiyo itaanza tarehe tatu mwezi huu.

Zaidi ya watoto Elfu Sitini wenye umri wa kati ya miezi Sita hadi miaka 15 watafikiwa na kampeni hiyo kwenye kambi moja iliyopo karibu na uwanja wa ndegeBanguina ile iliyoko Damala.

Dokta Evariste Pambigui kutoka kituo cha Damala amesema timu za WHO zilitembelea maeneo hayo na kubaini wagonjwa hao na wasiwasi mkubwa hivi sasa ni kwamba mlundikano wa watu kwenye kambi hizo za muda unaweza kuchochea kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo wa Surua.

UNICEF inasema kuwa chanjo na vifaa vya kutolea chanjo hiyo tayari vimeandaliwa na kwamba kampeni hiyo itachukua kati ya siku Tatu hadi Tano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031