Wakimbizi wa ndani Sudan Kusini waweka makao kwenye kituo UNMISS

Kusikiliza /

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Karibu mwezi mmoja tangu kuzuka kwa mapigano Sudan Kusini maelfu ya raia wamechukua hifadhi katika makambi ya mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNMISS mjini Juba na hawana dalili ya kurejea makwao.

Baadhi ya wakimbizi hao wa ndani wanaosema wanajihisi salama zaidi wakiishi kwenye maskani ya UNMISS kuliko majumbani kwao, wameanzisha biashara ya kuuza chai, chakula, mboga za majani na bidhaa nyingine muhimu kwa bei ya juu sana.

Mmoja wa wachuuzi hao amesema wanapata bidhaa hizo nje ya kambi kwa bei ya jumla , na wanauza kwa gharama kubwa ili kuhakikisha wanapata faida na biashara inaendelea. Amesema bidhaa hizo ni adimu kwa maeneo ya karibu na kambi na usafiri hauaminiki . Mbali ya UNMISS na wadau wengine kutoa msaada wa maji , magari binafsi yanatoa maji kwa matumizi yakpuka chakula na kuuza.

Mashirika ya Umoja wa mataifa nay ale yasiyo ya kiserikali NGO's yanashirikiana na UNMISS kutoa huduma muhimu kama malazi, huduma za afya, chakula na maji kwa wakimbizi hao wa ndani ambao wanakuwa changamoto wakati idadiyaoikiendelea kuongezeka kwenye maskani ya UNMISS.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930