UNHCR yazindua mfumo mpya wa Usajili kambini:Malawi

Kusikiliza /

Mtoto wa kike afanyiwa upelelezi katika kambi ya Dzaleka, UNHCR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limehitimisha jaribio la kwanza la mfumo mpya ambao unaotarajiwa kulisaidia kusajili na kulinda watu kwa njia bora zaidi. Mfumo huo utasaidia kuhakiki vitambulisho na misaada wanayohitaji watu walolazimika kuhama katika operesheni za UNHCR kote duniani. Grace Kaneiya na maelezo zaidi

 (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Zoezi la utambuzi kupitia kifaaa maalumu kilichoendelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na makampuni ya sekta binafsi lilifanywa kwa kuendesha vipimo katika kambi ya Dzaleka.

Zoezi hilo lililofanyika mwezi uliopita, limefanywa kwa kupitia hatua kadhaa ikiwemo kuchukua alama za vidole vya wahusika, upigaji wa picha na uchukuaji wa taarifa binafsi za mtu

Wataalamu wa UNHCR kwa hivi sasa wameanza kazi ya kupitia matokeo ya kazi hiyo na kufanya mapendekezo kwa ajili ya kuboresha zaidi wakati kazi hiyon itakapofanywa katika siku za usoni.

Steven Corliss, mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa  UNHCR amesema kuwa kile walichojifunza nchini Malawi kitatoa funzo kwa ajili ya kuendeleza miradi ya jinsi hiyo wakati itakapotekelezwa zaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930