Umekuwa ni muda mrefu tukitafuta dawa mujarabu ya mafanikio:Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akizungumza mjini Berlin, Ujerumani

Imekuwa ni muda mrefu saana watu wakitafakari na kukuna vichwa kupata mafanikio lakini utaratibu huo haujazaa matunda na sio endelevu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri wa kisayansi mjini Berlin, Ujerumani Alhamisi.

Bwana Ban amesema bodi hiyo itaongeza nguvu kwa Umoja wa mataifa katika kushughulikia changamoto za kimataifa kwa mtazamo jumuishi na wa jumla.

(Sauti ya Ban Ki-Moon)

Wajumbe wa bodi hii watashauri masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa maendeleo endelevu. Hii ni changamoto kubwa na kipaumbele kikubwa cha Umoja wa Mataifa."

Ameongeza kuwa dunia sasa imeingia katika zama mpya ambapo shughuli za binadamu zina athari za moja kwa moja katika mfumo wa maisha ya sayari yetu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930