Tunisia yapongezwa kwa kuanzisha katiba mpya, yapewa angalizo.

Kusikiliza /

Ravina Shamdasani

Msemaji wa Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani ameipongeza Tunisia kwa hatua ya kupitisha katiba mapya siku ya jumapili ambayo amesema inatafsiri matarajio ya utu, haki ya kijamii na ukombozi wa mtu binafsi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bi Shamdasani pia amepongeza mfano wa kujitoa katika mazungumzo na makubaliano ulioonyeshwa na taifa hilo ambao umewezesha mpito wa demokrasia nchini humo. Amesema mchakato wa katiba umenufaisha wigo wa ushiriki wa asasi za kiraia.

Hata hivyo ametoa angalizo kwa wanasiasa nchini Tunisia kuhakikisha kipindi kijacho cha mpito kinaendeshwa kwa amani,ujumuishwaji na uwazi. Msemaji huyo wa mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa amesema taifa hilo inabidi lihakikishe taasisi huru zilizoanzishwa katika katiba mpya kama vile taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu zinakuwa na nguvu na ili zikuze uwajibikaji na utawala wa sheria na kuheshimu kazi za biandamu.

Bi Shamsadani amesisistiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendela kusaidia Tunisia katika juhudi za taifa za kuanzisha jamii ya kidemokrasia na iliyo na uwazi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031