Sheria mpya Ukraine huenda zikaathiri vibaya mno haki za binadamu: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea kusikitishwa na sheria ilopitishwa mnanmo Alhamis wiki ilopita, ambayo inaweka masharti makali katika kufurahia haki za binadamu za msingi, zikiwemo haki na uhuru wa kujumuika na kujieleza, na kuweka adhabu kwa wanaozikiuka, ikiwemo kufungwa jela.

Bi Pillay amesisitiza haja ya kuwepo mazungumzo nchini Ukraine ili kuepusha kuenea kwa ghasia nchini humo, hususa kufuatia kuwekwa kwa sheria mpya ambayo haiambatani na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Bi Pillay amesema ghasia za hivi karibuni mjini Kieve ambazo ziliripotiwa kusababisha majeruhi wengi zinasikitisha mno, na kutoa wito kwa kwa pande zote husika kufanya mazungumzo, kwani kadri zinapochelewa kufanya hivyo, ndivyo inavyokuwa hata vigumu zaidi kuutatatu mzozo uliopo sasa.

Amependekeza pia kuwa, mazungumzo hayo yawe jumuishi na endelevu, huku akizingatia kwamba serikali tayari imeanza tena juhudi za kuanzisha mazungumzo na viongozi wa upinzani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031