Senegal yakaribia kutokomeza mbun'go

Kusikiliza /

Madume tasa ya mbung’o huachiwa hewani mara ili kupunguza uzao wa wadudu hao

Mradi unaotekelezwa na shirika la kilimo na chakula duniani, FAO nchiniSenegalwenye lengo la kutokomeza mbung'o umeanza kuonyesha dalili ya kushinda vita dhidi ya wadudu hao hatari kwa mifugo.

Meneja mradi huo kutoka Wizara ya Mifugo Baba Sall amesema tangu kuanza kwa mradi mwaka 2012, idadi ya wadudu hao imepungua kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la Niayes karibu na mji mkuu Dakar.

Amesema eneo hilo lina mazingira bora kwa mbung'o kuzaliana na hivyo kusababisha ugonjwa wa homa ya malale kwa mifugo hususan ng'ombe wa maziwa na wale wa nyama.

Sall amesema mradi huo unaotumia teknolojia ya kuzalisha madume tasa ya mbung'o ambayo yanapokutana na mbung'o jike hayawezi kupata watoto umepunguza idadi ya mbung'oporiwarukao kwa asilimia 99 ndani ya miezi Sita.

Amesema mbinu hiyo ni rafiki kwa mazingira kwani hakuna dawa inayotumika kwa wanyama kuwakinga na wadudu hao. Wadau wengine katika mradi huo ni pamoja na shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, Marekani na Ufaransa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031